Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira Mhe. Khamis Hamza Khamis ameitaka jamii kuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu ya kutunza na kuhifadhi mazingira ili kuwa na kizazi chenye uelewa na kuthamini mazingira hususan uchumi wa bluu.
Ameyasema hayo leo tarehe 22/10/2024 wakati wa ufunguzi rasmi wa warsha ya Kimataifa wa Jumuiya ya Ukanda wa Bahari ya Hindi (IORA) katika Hotel Seascape, Dar es salaam iliyoratibiwa na Chuo Kikuu Mzumbe na kushirikisha nchi ambazo zimezunguka Ukanda wa bahari ya Hindi
Naibu Waziri Khamis, ametoa rai kwa wadau wote wa ukanda wa bahari ya Hindi (IORA), kuhakikisha kwamba jamii inapata uelewa na elimu sahihi ya kuhusu kutunza Mazingira
“Kwetu sisi wasomi twendeni tukatoe elimu kwa jamii kuhusu kutunza Mazingira, jamii yetu haina uelewa wa kutosha kuhusu masuala ya Ikolojia, kaboni na namna bora ya utunzaji wa mazingira twende tukawaelimishe watu jinsi ya kuvuna kaboni” alisisitiza Mhe Khamis.
Amesema uelewa wa masuala ya Kaboni na matumizi sahihi ya rasilimali za bahari kupitia uchumi wa bluu ni muhimu kwa jamii inayozunguka mazingira ya pwani kwa kuwa husaidia katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na kutoa kwa Jumuiya ya Ukanda wa Bahari ya Hindi (IORA) kuweka nguvu zaidi katika kutoa elimu. “Tunaomba mtusaidie kuelimisha jamii ili kutunza Mazingira.”Alisitiza Mhe Khamis
Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha, amesema wakati ni sasa wa kuunganisha nguvu za wasomi, watafiti na wanamazingira kuendelea kuhimiza uhifadhi wa mazingira na kusisitiza matumizi sahihi ya uchumi wa bluu kama njia ya kulinda mazingira na chanzo cha maendeleo endelevu kwa vizazi vijavyo.
Nchi au ukanda unaohusishwa na IORA (Indian Ocean Rim Association - Jumuiya ya Ukanda wa Bahari ya Hindi) umeanza kugundua na kutumia faida za "kaboni ya bluu" katika juhudi zao za kuhifadhi mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa njia endelevu. Alifafanua Prof.Mwegoha.
Naye mratibu wa warsha hiyo Dkt. Saida Fundi kutoka Chuo Kikuu Mzumbe amepongeza IORA na kuelezea namna inavyo pambana kutunza Mazingira na kuelimisha jamii kwa ujumla.
"Ni muhimu jamii ikaelimika na kuwa na uelewa mpana juu ya mazingira ili iwe rahisi kuyatunza na kuhifadhi kwa maendeleo ya vizazi vijavyo" amesisitiza Dkt. Saida
Mkutano huo umejumuisha wawakilishi kutoka nchi mbalimbali kutoka ukanda wa bahari ya buluu ikiwa ni pamoja na Australia, Bangladesh, Comoros, France, India, Indonesia, Iran, Kenya, Madagascar, Malaysia, Maldives, Mauritius, Mozambique, Oman, Seychelles, Singapore, Somalia, South Africa, Sri Lanka, Tanzania, Thailand, United Arab Emirates, Yemen.
Mgeni Rasmi wa Warsha ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira Mhe. Khamis Hamza Khamis akiwasili Hoteli ya Seascape kwa ajili ya kufungua Warsha ya Kimataifa ya IORA (Indian Ocean Rim Association) inayolenga kuibua fursa za kiuchumi na uhifadhi wa rasilimali Bahari. Warsha hii imeratibiwa na Chuo Kikuu Mzumbe kwa kushirikana na IORA.
Mgeni Rasmi wa Warsha ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira Mhe. Khamis Hamza Khamis akisalimiana na waratibu wa warsha alipo wasili katika Hoteli ya Seascape kwa ajili ya kufungua Warsha ya Kimataifa ya IORA (Indian Ocean Rim Association) inayolenga kuibua fursa za kiuchumi na uhifadhi wa rasilimali Bahari. Warsha hii imeratibiwa na Chuo Kikuu Mzumbe kwa kushirikana na IORA.
Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Saida Fundi ambaye ni mratibu wa Warsha kwa upande wa Chuo Kikuu Mzumbe, akieleza ushiriki wa Chuo katika Warsha ya Kimataifa ya IORA (Indian Ocean Rim Association) inayolenga kuibua fursa za kiuchumi na uhifadhi wa rasilimali Bahari. Warsha hii imeratibiwa na Chuo Kikuu Mzumbe kwa kushirikana na IORA.
Makumu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha akitoa hotuba kwa Mgeni Rasmi wakati wa Warsha ya Kimataifa ya IORA (Indian Ocean Rim Association) inayolenga kuibua fursa za kiuchumi na uhifadhi wa rasilimali Bahari. Warsha hii imeratibiwa na Chuo Kikuu Mzumbe kwa kushirikana na IORA.
Kaimu Mkurugenzi, Uchumi wa Buluu wa Usimamizi wa Wavuvi – IORA Sekretarieti, Bi. Zelda Vrolick akieleza lengo pamoja na shughuli zinazotekelezwa na IORA wakati wa Warsha ya Kimataifa ya IORA (Indian Ocean Rim Association) inayolenga kuibua fursa za kiuchumi na uhifadhi wa rasilimali Bahari. Warsha hii imeratibiwa na Chuo Kikuu Mzumbe kwa kushirikana na IORA.
Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kikanda Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Talha M. Waziri akizungumza wakati wa Warsha ya Kimataifa ya IORA (Indian Ocean Rim Association) inayolenga kuibua fursa za kiuchumi na uhifadhi wa rasilimali Bahari. Warsha hii imeratibiwa na Chuo Kikuu Mzumbe kwa kushirikana na IORA.
Kaimu Naibu Makumu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe – Taaluma, Utafiti na Ushauri, Prof. Eliza Mwakasangula akitoa salamu za Shukrani wakati wa Warsha ya Kimataifa ya IORA (Indian Ocean Rim Association) inayolenga kuibua fursa za kiuchumi na uhifadhi wa rasilimali Bahari. Warsha hii imeratibiwa na Chuo Kikuu Mzumbe kwa kushirikana na IORA.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira Mhe. Khamis Hamza Khamis akizungumza wakati wa Warsha ya Kimataifa ya IORA (Indian Ocean Rim Association) inayolenga kuibua fursa za kiuchumi na uhifadhi wa rasilimali Bahari. Warsha hii imeratibiwa na Chuo Kikuu Mzumbe kwa kushirikana na IORA.
Washiriki wa Warsha ya Kimataifa ya IORA (Indian Ocean Rim Association) wakiwa katika Warsha hiyo yenye lengo la kuibua fursa za kiuchumi na uhifadhi wa rasilimali Bahari. Warsha hii imeratibiwa na Chuo Kikuu Mzumbe kwa kushirikana na IORA.
Picha ya pamoja ya Mgeni Rasmi wa Warsha ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira Mhe. Khamis Hamza Khamis na waratibu wa Warsha ya Kimataifa ya IORA (Indian Ocean Rim Association) inayolenga kuibua fursa za kiuchumi na uhifadhi wa rasilimali Bahari. Warsha hii imeratibiwa na Chuo Kikuu Mzumbe kwa kushirikana na IORA.