Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kupitia Idara ya Kazi imetoa elimu juu ya utekelezaji wa sheria za kazi kwa wadau wa sekta ya usafirishaji nchini ikiwa ni moja ya jukumu la idara hiyo.
Akizungumza katika mafunzo hayo Mkoani Songwe Kamishna wa Kazi Ofisi hiyo Suzan Mkangwa, amesema lengo la mafunzo hayo ni kutoa elimu kwa waajiri ili kuendelea kusimamia sheria za sheria na kupunguza ama kuondoa malalamiko ya wafanyakazi ya ukiukwaji kwa sheria za kazi.
"Ni muhimu kwa waajiri kujua sheria ili waweze kutekeleza vizuri wajibu wao kwa wafanyakazi wanao wasimamia" amesema.
Aidha, Kamishna Mkanngwa amesema mafunzo hayo yataendelea kuimarisha utekelezaji wa sheria za kazi nchini hususan sekta ya usafirishaji ambayo ni moja ya sekta muhimu katika kukuza uchumi wa nchi.
Kamishna wa Kazi Msaidizi, Ukaguzi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na wenye Ulemavu Rehema Moyo akitoa elimu kwa wadau wa sekta ya usafirishaji juu ya mada inayohusu Usimamizi wa sheria za kazi katika mafunzo yaliyofanyika mkoani Songwe
Aidha lengo la mafunzo hayo ni kutoa elimu kwa waajiri ili kuendelea kusimamia sheria za sheria na kupunguza ama kuondoa malalamiko ya wafanyakazi ya ukiukwaji kwa sheria za kazi.
Kamishna wa Kazi Msaidizi Ifisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Jira na Wenye Ulemavu Andrew Mwalwisi akitoa elimu juu ya sheria za kazi na kanuni za muongozo kuhusu utekelezaji wa sheria kwa wadau wa sekta ya usafirishaji nchini katika mafunzo yaliyofanyika mkoani Songwe.