Rais na Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Kampuni ya Barrick, Mark Bristow, katikati washirikiana na Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini, Mwita Waitara kukata utepe katika hafla ya uzinduzi wa shule hiyo.
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Kampuni ya Barrick, Mark Bristow akifunua kitambaa kuashuria uzinduzi wa shule hiyo iliyojengwa na mgodi wa North Mara.
**
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Kampuni ya Barrick, Mark Bristow. amekabidhi kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime shule ya msingi mpya ya kisasa ya Kenyangi iliyojengwa na Mgodi wa Dhahabu wa North Mara.
Shule hiyo imejengwa katika kijiji cha Matongo, jirani na mgodi huo unaoendeshwa na Kampuni ya Barrick kwa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia Kampuni ya Twiga Minerals.
Mgodi wa North Mara umejenga shule hiyo ili kuhamisha Shule ya Msingi Kenyangi kwa ajili ya kupisha upanuzi wa shughuli zake.
“Ninaishukuru jamii ya hapa kwa ushirikiano mkubwa uliotuwezesha kufanikisha utekelezaji wa mradi huu, na ninawatakia kila la heri wanafunzi wanaokuja kusoma hapa,” amesema Mark Bristow katika hafla ya kukabidhi shule hiyo.
Amesisitiza umuhimu wa uwekezaji kwenye sekta ya elimu kwa maendeleo ya jamii inayozunguka mgodi huo na bara la Afrika kwa ujumla. “Kusherekea uwekezaji wa shule hii ni kusherekea Afrika ya baadaye,” amesema.
Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini, Mwita Waitara, amemshukuru Mark Bristow na kumueleza kuwa shule hiyo ni miongoni mwa miradi mikubwa ya kijamii iliyojengwa kutokana na fedha za Mgodi wa North Mara.
“Mark Bristow, tunakushukuru sana kwa shule hii, na hii ni miongoni mwa shule bora katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, watoto watasoma katika mazingira mazuri,” amesema Waitara.
Naye Diwani wa Kata ya Matongo, Godfrey Kegoye, ameshukuru akisema ubora wa shule hiyo utachochea ukuaji wa taaluma kwa wanafunzi.
“Tunamshukuru sana Rais wa Barrick Mark Bristow, kwa sababu vitu vyote anavyoahidi anavitekeleza kwa vitendo, tunamwombea baraka kwa Mungu,” amesema Kegoye.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kenyangi, Hadija Nusura naye ameshukuru akisema “Mgodi umetujengea shule nzuri sana, kwa kweli tunapaswa kujivunia mgodi huu.”
Awali, Mark Bristow, alipata fursa ya kujinoea miundombinu ya shule hiyo na kupanda mti wa asili kama ishara ya Mgodi wa North Mara kuunga juhudi za uhifadhi wa mazingira.
Hafla ya kukabidhi shule hiyo ilihudhuriwa pia na Meneja wa Barrick nchini Tanzania, Melkiory Ngido, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Paragia Balozi, Meneja Mkuu wa Mgodi wa North Mara, Apolinary Lyambiko, Wafanyakazi wa Barrick, Madiwani, Wenyeviti wa vijiji, wazee wa mila na wanafunzi.
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Kampuni ya Barrick, Mark Bristow (kulia) akibadilishana mawazo na Meneja wa Mgodi wa North Mara,Apolinary Lyambiko wakati wa hafla hiyo.
Meneja wa Mgodi wa North Mara,Apolinary Lyambiko akimuonyesha Rais na Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Kampuni ya Barrick, Mark Bristow na wafanyakazi Waandamizi wa kampuni mazingira ya shule hiyo.
Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na Mbunge Waitara,Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick Mark Bristow na wafanyakazi wa Barrick.
Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na Mbunge Waitara,Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick Mark Bristow na wafanyakazi wa Barrick.
Wazee wa kimila katika picha ya pamoja na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick,Mark Bristow na Mbunge wa Tarime Vijijini,Mwita Waitara.
Wanafunzi na walimu wakicheza ngoma kwa furaha wakati wa hafla hiyo
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Kampuni ya Barrick, Mark Bristow akishiriki zoezi la kupanda mti wa kumbukumbu wakai wa uzinduzi huo
Sehemu ya wageni waalikwa na wafanyakazi wa Barrick katika hafla hiyo