Breaking

Saturday, 19 October 2024

BALOZI BWANA AMKABIDHI KATIBU MTENDAJI WA SEKRETARIETI YA SADC BARUA YA UTEUZI WA KIONGOZI MKUU WA TIMU YA SADC YA WAANGALIZI WA UCHAGUZI


Na: Fortunatus Charles Kasomf Gaborone Botswana

Balozi wa Tanzania anayehudumu katika nchi za Jamhuri Afrika Kusini, Falme ya Lesotho, Jamhuri ya Botswana na Sekretariati ya Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) Mhe. James G. Bwana ( kushoto) akimkabidhi Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya SADC Mhe. Elias Magosi ( kulia) barua ya uteuzi wa kiongozi Mkuu wa Timu ya SADC ya Waangalizi wa Uchaguzi Mkuu wa Botswana, utakaofanyika tarehe 30 Oktoba, 2024.

Barua hiyo imesainiwa na Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye amemteua Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda, kuwa Kiongozi Mkuu wa Timu ya SADC ya Uangalizi wa Uchaguzi huo Mkuu wa Botswana.

Mhe. Pinda anawasili nchini Botswana, Alasiri ya leo tarehe 19 Oktoba,2024 tayari kutekeleza majukumu hayo.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages