Breaking

Sunday 29 September 2024

Waziri Silaa Awasisitiza Waumini Kujiandikisha Kupiga Kura

WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe.Jerry Silaa amewaomba viongozi wa kanisa kuwaasa waumini wao kutenga muda wa kujiandikisha katika daftari la wapiga kura ili wapate nafasi ya kushiriki kuchagua viongozi kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Ombi hilo amelitoa leo Septemba 29,2024 katika harambee ya ujenzi wa  kanisa la KKT Kigezi-Chanika Jijini Dar es Salaam.

 Aidha amesema waumini wa kanisa wanaweza pia kuomba nafasi za uongozi,kwa lengo la kupata viongozi wenye hofu ya mungu ili kuleta maendeleo bora na ustawi wa jamii.

Pamoja na hayo amesema jukumu la uraia linajumuisha kuchagua na kuchaguliwa kuwa viongozi  kwa ajili ya wananchi wote ambapo upatikanaji wa huduma ya shule, zahanati na mengine yanahusiana na uwepo wa viongozi wanaopatikana kupitia chaguzi.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages