Breaking

Thursday, 19 September 2024

SERIKALI KUJENGA VITUO VYA ZANA ZA KILIMO



Na Mwandishi wetu, Ruvuma

SERIKALI imetangaza kujenga vituo vya zana za kilimo nchi nzima na kuanza kugawa ruzuku ya mbegu za mahindi.

Pia Waziri wa Kilimo mhe Husein Bashe (mb) amesena atakula sahani moja na wafanyabiashara vishoka wanaonyonya wakulima.

Hayo yameelezwa leo katika muendelezo wa ziara ya kikazi ya Waziri Bashe akiwa Mkoani Ruvuma katika kituo cha ununuzi wa mahindi Madaba.

Amesema Serikali inatambua adha wanayokutana nayo wakulima kutokana na uhaba wa Zana za kilimo, na maumivu wanayokutana nayo katika kukodi Trekta, pawatila, ulanguzi katika mbegu, mbolea.

Amesema, serikali katika katika kuhakikisha sekta ya kilimo inakuwa na tija na kufika masoko ya kimataifa na kuifanya sekta hiyo kuinua uchumi imeamua kuwekeza.

“Rais huyu kwa nia ya dhati kabisa ameamua na kutenga fedha za kujenga vituo vya zana za kilimo zaidi ya 45 nchi nzima,”amesema.

Ameeleza katika vituo hivyo kutakuwa na zana za kilimo kama matrekta na zana zake zikiwemo plau, haro, planters, boom sprayers na tela za kusafirishia mizigo pamoja na Combine Harvester.

Waziri Bashe ameitaja mikoa itakayonufaika na awamu ya kwanza ya ujenzi huo kuwa ni Mwanza,Simiyu,Geita,ShinyangKigoma,Mara,Tabora,Singida,Katavi, Shinyanga,Mbeya, Njombe, Ruvuma, Tanga, Dodoma.

“Tumetambua kuwa wakulima wanakodishiwa zana hizo kutoka sh. 60,000 hadi 120,000 hii si sawa na kuumiza wakulima na hawawezi kuona tija katika kilimo serikali imeamua italeta zana hizo ikiwemo matrekta na wakulima watakodi kwa bei elekezi ya sh 35,000 hadi 40,000 haitazidi hapo,”amesema.

Amesema mwakani pia serikali itasambaza mashine za kusafishia mahindi, mtama na mazao mengine lengo ni kuona bidhaa hizo zinakidhi viwango vya soko la kimafaifa na itatenga fedha ya kununu nafasi zisizo an ubora kwa ajili ya chakula cha mifugo ili kuwapungizia hasara wakulima.

Pia ameeleza lengo la serikali kuanza kutoa ruzuku katika bei ya mahindi.

“Tunajua mapambano yaliyopo soko la kimataifa niwahakikishie tunaleta ruzuku katika bei ya mbegu za mahindi, ili kupambana na uhuni unaoendelea.

“Kuna watu wanapaka rangi katika mbegu za mahindi na kuziweka sokoni, tutaondoa mbegu zote ambazo hazikidhi,”amesema Waziri Bashe.

Pia ametangaza vita na wafanyabiashara wanaowanyonya wakulima hususani wanaonunua mazao kwa bei ya chini na wanaouza pembejeo za kilimo kwa bei ya ulanguzi.

“Wapo wafanyabishara wanaonya na kula jasho la wakulima bila uoga bei elekezi ya mahindi ni sh 700 kg lakini wao wananunua kwa sh 300, mpunga kg 1 ni sh 900 kg 100 sh 81,000 wao wananunua kg 1 kwa sh 600 hii hatutajubali.

“Sina tatizo na wafanyabishara lakini sitavumilia unyonyaji uliopitiliza tutajenga maghala kila sehemu hawataki kununua naiagiza Mamlaka ya Hifadhi ya Chakula (NFRA), kuhakikisha inanunua mazao hayo nchi nzima mpaka kabla ga msimo wa kilimo kuisha,”amesema.

Naye Mbunge wa Madaba Dkt. Joseph Mhagama, akizungumza kwa niaba ya wananchi, ameishukuru serikali kwa hatua zinazo endelea, ikiwepo ujenzi wa ghala kubwa katika kata ya Madaba na ujenzi wa vituo 9 vya zana za kilimo mkoni humo.

“ Sisi Madaba tumejiandaa kupokea neema hiyo na tumetenga zaidi ya hekari 25,000 za ardhi kupisha eneo la zana za kilimo na mashamba ya mbegu,”amesema.

Mwisho




Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages