Breaking

Thursday 12 September 2024

NAIBU WAZIRI PINDA AKABIDHI HUNDI YA MIL 45 KUTOKA CRDB KWA WAJASIRIAMALI MPIMBWE

Na Munir Shemweta, WANMM MLELE

Mbunge wa jimbo la Kavuu na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda amekabidhi hundi ya shilingi milioni 45 kwa vikundi vitatu vya wajasiriamali wa halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi kutoka benki ya CRDB kuvijengea uwezo.

Mhe Pinda amekabidhi hundi hiyo tarehe 12 Sept 2024 wakati akifungua semina ya siku moja ya kuvijengea uwezo vikundi vya wajasiriamali wanawake na vijana kunufaika na programu ya IMBEJU katika kata za halmashauri ya Mpimbwe wilayani Mlele mkoa wa Katavi iliyofanyika kata ya Majimoto.

Vikundi vilivyokabidhiwa kiasi hicho cha fedha ni Nguvumoja Kashishi, Imani Kashishi pamoja na kikundi kingine kitakachokidhi vigezo vya kuwezeshwa.

Akizungumza wakati wa kuzindua semina hiyo Mhe. Pinda amesema Ili kuendesha biashara kisasa ni lazima wajasiriamali wapate ushauri na mafunzo kutoka kwa wataalamu.

Ameeleza kuwa, taasisi za fedha kama CRDB ni miongoni mwa sehemu ya uhakika ambayo mjasiriamali anaweza kupata elimu ya fedha ya uhakika ili kufanikisha mipango ya biashara.

Amewataka wajasiriamali wa Mpimbwe kutumia fursa inayolingana na uwezo wao binafsi na siyo kusikia tu benki inatoa mitaji wezeshi na kulazimika hata kudanganya ili kukopa fedha pasipo mikakati makini ya kuzitumia.

Ameishukuru CRDB kupitia taaasisi yake ya CRDB Foundation kwa ubunifu wa kuwafikia wajasiriamali wadogo hata waliopo pembezoni kama vile Mpimbwe.

"Hii si jambo dogo kwa taasisis inayojiendesha kibiashara kutenga bajeti ya kuelimisha wananchi na kuwapa mitaji wrzeshi" alisema Mhe. Pinda

Washiriki wa semina hiyo ya siku moja wametoka kata za Kasansa, Mamba, Majimoto, Mwamapuli, Chamalendi, Mbede, Ikuba, Usevya pamoja na Kibaoni katika halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi.

Mbunge wa jimbo la Kavuu na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akikabidhi hundi ya shilingi milioni 45 kwa vikundi vitatu vya wajasiriamali wa halmashairi ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi kutoka benki ya CRDB kuvijengea uwezo.
Mbunge wa jimbo la Kavuu na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda azungumza na wajasiriamali wa halmashairi ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi wakati wa semina ya kuwajengea uwezo iliyoendeshwa na CRDB kupitia program ya Imbeju tarehe 12 Sept 2024.

Sehemu ya washiriki wa semina ya kuwajengea uwezo wajasiriamali wa halmashauri ya Mpimbwe iliyoendeshwa na CRDB kupitia program ya Imbeju tarehe 12 Sept 2024.
Mbunge wa jimbo la Kavuu na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akiwa katika picha ya pamoja na wajasiriamali wa vikundi alivyovikabidhi hundi ya mil 45 wakati wa semina ya kuwajengea uwezo kata ya Majimoto halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi tarehe 12 Sept 2024
Mbunge wa jimbo la Kavuu na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akiwa na washiriki semina ya kuwajengea uwezo wajasiriamali wa halmashairi ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi tarehe 12 Sept 2024
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages