Breaking

Saturday 28 September 2024

GAUWASA WAJA DAWASA "KUCHOTA MADINI" HUDUMA KWA WATEJA



Watumishi kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Gairo (GAUWASA) wamefanya ziara ya mafunzo Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kwa lengo la kujifunza zaidi na kubadilishana uzoefu wa uendeshaji na usimamizi bora wa huduma za Majisafi na Usafi wa mazingira.

Katika ziara hiyo wametembelea Mtambo wa uzalishaji maji Ruvu Juu pamoja na mitambo ya kisasa ya kuchakata takatope kujionea na kujifunza jinsi DAWASA inavyotekeleza shughuli za uzalishaji na usambaji Majisafi pamoja na huduma za usafi wa mazingira.





Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages