Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akiwa na viongozi wakitembelea mradi wa bandari ya Uvuvi uliopo Kilwa Masoko wilayani Kilwa wakati wa ziara Maalum Mkoani humo yenye lengo la kukagua utekekelezaji wa Miradi ya maendeleo chini ya kauli mbiu isemayo "Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone".
Na.Mwandisi Wetu.
WAZIRI wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt Selemani Jafo amewashauri wananchi wa wilaya ya Kilwa kushikamana na kusimamia Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa wilayani humo ikamilike kwa wakati na iendane na gharama halisi ili kutimiza Dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kuhakikisha wananchi hao wananufaika na miradi hiyo.
Dkt.Jafo ameyasema hayo wakati wa ziara Maalum Wilaya ya Kilwa, Mkoa wa Lindi yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo na kuongea na Wananchi wa Maeneo hayo ikiongozwa na Kauli Mbiu isemayo "Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone".
Waziri Jafo ameliagiza Shirika la Umeme (TANESCO ) kuhakikisha mradi wa nyumba za walimu (Two in One) zilizopo Kata ya Somanga zinapata umeme na Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kuhakikisha wanajenga barabara nzuri ndani ya miezi miwili ili kuweka mazingira bora ya kuishi na kufanya kazi kwa ufanisi kwa Walimu hao.
"Naielekeza Mamlaka ya Maji Kilwa Masoko (KIMUWASA) inayosimamia Mradi wa maji katika vijiji vya Mavuji, Nangurukuru, Singino, Kivinje, Mpara na Masoko uliopo Wilayani Kilwa kusimamia Mradi huo kukamilifu na kuandaa Mpango unaonesha Mradi huo utakamilika lini na kuwasilisha katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi ndani ya Wiki mbili (2) ili kuhakikisha Mradi huo unaleta manufaa yanayotarajiwa kwa Wananchi wa Kilwa."amesisitiza Dkt.Jafo
Aidha, Dkt Jafo amebainisha kuwa ujenzi wa Mradi wa Bandari ya Uvuvi unaolenga kurahisisha upatikanaji wa Samaki, Soko na kukuza biashara uchumi kwa ujumla pamoja ujenzi wa Kituo cha Afya cha Njinjo, Kipimimbi unaendelea kwa kasi , unaendana na gharama iliyopangwa na hivyo kufikia malengo yanayotarajiwa na Wananchi wa Kilwa.
Akiongea na Wananchi wa Kipimindi Wilayani Kilwa Dkt Jafo amewapongeza wananchi wa Wilaya hiyo kwa kutumia Mfumo wa stakabadhi gharani hususani katika mazao ya ufuta na mbaazi na kupata mafanikio makubwa katika kuuza mazao hayo ndani na nje ya nchi kwa bei inayoridhisha na kuchangia katika kukuza biashara na kuongeza pato la Taifa.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Zainab Telack ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo Mkoani humo inayolenga kuleta manufaa makubwa kwa Wananchi wa Mkoa huo na kuwaomba kutumia fursa za miradi hiyo ili kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya Mkoa huo na Taifa kwa ujumla.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili mkoani Lindi kwa jaili ya kufanya ziara Maalum Mkoani humo yenye lengo la kukagua utekekelezaji wa Miradi ya maendeleo chini ya kauli mbiu isemayo "Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone".
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akizungumza na Viongozi wa Wilaya ya Kilwa, Walimu na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Somanga iliyopo Kata ya Somanga, alipotembelea Shule hiyo kujionea Mradi wa ujenzi wa nyumba za Walimu (two in one) wakati wa ziara Maalum Mkoani humo yenye lengo la kukagua utekekelezaji wa Miradi ya maendeleo chini ya kauli mbiu isemayo "Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone".
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akiwa na viongozi wakitembelea mradi wa bandari ya Uvuvi uliopo Kilwa Masoko wilayani Kilwa wakati wa ziara Maalum Mkoani humo yenye lengo la kukagua utekekelezaji wa Miradi ya maendeleo chini ya kauli mbiu isemayo "Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone".
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akiwa na viongozi wakikagua ujenzi wa Mradi wa Maji mavuji,Nangurukuru,Singino,Kivinje,Mpara ,Masoko uliopo wilayani Kilwa wakati wa ziara Maalum Mkoani humo yenye lengo la kukagua utekekelezaji wa Miradi ya maendeleo chini ya kauli mbiu isemayo "Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone".
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akizungumza na wananchi wa Kipimindi wilayani Kilwa baada ya kutembelea ujenzi wa Kituo cha Afya cha Njinjo Mkoani humo wakati wa ziara Maalum Mkoani humo yenye lengo la kukagua utekekelezaji wa Miradi ya maendeleo chini ya kauli mbiu isemayo "Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone".
Wednesday, 18 September 2024
DKT.JAFO AAGIZA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI KILWA KUKAMILIKA KWA WAKATI
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990