Breaking

Saturday, 10 August 2024

WATANZANIA WAANDAMANA KENYA KUOMBEA AMANI

 

Mamia ya waumini kutoka Tanzania wa Kanisa la Newlife and Player Center lililopo Mombasa nchini Kenya wamefanya maandamano ya amani kanisani hapo Kilifi leo Agosti 10,2024 kuiombea amani nchi yao (Tanzania) kufuatia uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu pamoja na uchaguzi mkuu mwakani.

Nabii wa kanisa hilo kutoka Tanzania, Utukufu kwa bwana Peter, amesema kusanyiko hilo linatokana na imani waliyonayo waumini hao kwa kanisa hilo ambalo limekuwa likiwapatia huduma ya pamoja na mambo mengine, kuwaponya maradhi mbalimbali na kuimarisha familia zao.

"Kwahiyo tunaamini silaha hutengenezwa wakati wa amani na kutumika wakati wa vita. Hivyo leo hii tunaomba amani itakayoendelea kutuunganisha watanzania sasa na wakati huo wa uchaguzi.

"Tunaunga mkono juhudi za Rais wetu mama Samia Suluhu Hassan za kuendelea kuimarisha amani,umoja,upendo na mshikamano katika nchi yetu," amesema Nabii na kusisitiza kwamba:
Imekuwa ikishuhudiwa katika baadhi ya mataifa kwamba baada ya uchaguzi amani inakua imetoweka, hali ambayo waumini hao wamechukua hatua ya kuizuia kupitia ibada.

Kwa niaba ya wenzake, mtanzania kutoka Bomang'ombe mkoani Kilimanjaro Rose Godfrey ambaye kupitia maombi ya kiongozi mkuu wa Kanisa hilo, Ezekiel Odero alipona saratani ya kizazi, amesema waumini hao wanaamini nguvu ya maombi, Tanzania itaendelea kuwa na amani.


Muinjilisti wa Kanisa la Newlife and Player Center Ezekiel Odero, akiendesha maombi yaliyohudhuriwa na watanzania ili kuiombea nchi amani katika chaguzi zijazo.
Muinjilisti wa Kanisa la Newlife and Player Center Ezekiel Odero, akiendesha maombi yaliyohudhuriwa na watanzania ili kuiombea nchi amani katika chaguzi zijazo.
Waumini wa Kanisa la Newlife and Player Center wakiomba maombi mbalimbali ikiwemo kuiombea Tanzania amani kwenye chaguzi zijazo.
Waumini wa Kanisa la Newlife and Player Center wakiomba maombi mbalimbali ikiwemo kuiombea Tanzania amani kwenye chaguzi zijazo.



Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages