Breaking

Thursday 22 August 2024

VIJIJI 63 VYAFANYIWA MIPANGO YA MATUMIZI YA ARDHI CHAMWINO

Makamu wa Rais Mhe. Dkt Philip Isdori Mpango akisalimiana na viongozi mara baada ya kuwasili kwenye kijiji cha Mpwayungu wilaya ya Chamwino wakati wa kilele cha ziara yake ya siku nne mkoa wa Dodoma tarehe 22 Agosti 2024.

*********************

Na Munir Shemweta, WANMM CHAMWINO

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda amesema jumla ya vijiji 63 kati ya vijiji 73 vilivyokuwa katika mpango kwenye wilaya ya Chamwino mkoa wa Dodoma vimefanyiwa mipango ya matumizi bora ya ardhi.

Aidha, vijiji 10 vilivyosalia viko katika mchakato wa kufanyiwa mipango ya matumizi bora ya ardhi katika wilaya hiyo ya Chamwino.

Mhe. Pinda amesema hayo tarehe 22 Agosti 2024 katika mkutano wa hadhara kwenye kijiji cha Mkwayungu wilayani Chamwino wakati kilele cha hitimisho ya ziara ya siku nne ya Makamu wa Rais Mhe. Dkt Philip Isdori Mpango kukagua miradi ya maendeleo kwenye mkoa wa Dodoma.

Kwa mujibu wa Mhe. Pinda, mpaka kufikia Disemba, 2024 vijiji vyote wilaya ya Chamwino vitakuwa imeshafanyiwa mipango wa matumizi bora ya ardhi na kusisitiza kuwa, kimsingi migogoro ya mipaka ya vijiji imetatuliwa kwa kiwango kikubwa.

"Mipango ya matumizi bora ya ardhi katika vijiji inaondoa changamoto kati ya mwananchi na mwananchi,wilaya na wilaya pamoja na changamoto nyingine za ardhi katika maeneo mengine". Amesema Mhe. Pinda.

Aidha, ameongeza kuwa, kiasi cha Tshs. 1.5 bil kimetengwa na kutumika kwenye mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi ( LTIP) katika wilaya ya CHAMWINO.

Sambamba na hilo, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amesema,

Vijiji 27 vimepimwa na kutayarishiwa vyeti ya vijiji huku vipande vya ardhi vilivyotambuliwa kwa ajili ya kutoa Haki za hatimiliki za Kimila ( CCROs) ni 20,455.

Makamu wa Rais Mhe. Dkt Philip Isdori Mpango akisalimiana na viongozi mara baada ya kuwasili kwenye kijiji cha Mpwayungu wilaya ya Chamwino wakati wa kilele cha ziara yake ya siku nne mkoa wa Dodoma tarehe 22 Agosti 2024
Makamu wa Rais Mhe. Dkt Philip Isdori Mpango akizungumza mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika scheme ya umwagiliaji katika kijiji cha Ndogowe wilayani Chamwino mkoa wa Dodoma tarehe 22 Agosti 2024. Kulia ni Naibu Waziri wa Ardhi Mhe, Geophrey Pinda.
Makamu wa Rais Mhe. Dkt Philip Isdori Mpango akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika scheme ya umwagiliaji katika kijiji cha Ndogowe wilayani Chamwino mkoa wa Dodoma tarehe 22 Agosti 2024. Kushoto aliyesimama ni Naibu Waziri wa Ardhi Mhe, Geophrey Pinda. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages