Breaking

Tuesday, 27 August 2024

TBS YASHIRIKI MAONESHO YA KITAIFA YA USALAMA BARABARANI MKOANI DODOMA


SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea kutoa elimu ya ubora katika Maonesho ya Kitaifa ya Usalama wa Barabarani yaliyofanyika viwanja vya Jamhuri Dodoma ambapo wameeleza ni jinsi gani wanahakikisha matumizi sahihi ya vipuli vya magari pamoja na uingizaji wa magari used yakiwa salama nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 26, 2024 katika Maonesho hayo, Meneja wa Viwango, Mhandisi Yona Afrika amesema TBS ndio wakaguzi wa magari yaliyotumika nchini kuwa ni salama, pia wanakagua vipuri vya magari kama breki na ukaguzi wa mafuta salama ya magari.

Amesema wamekuwa wakiandaa viwango vya mafuta salama ya magari nchini ili kuhakikisha magari yanayotumika nchini yanatumia mafuta salama ya magari na kuondokana na changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza kwenye magari pindi wanapotumia mafuta ambayo si salama.

"TBS tunahakikisha magari yote yanayoingia nchini, yanaingia yakiwa salama na yanachangia kwa kiasi kikubwa usalama barabarani ambapo pia vipuri vya kwenye magari tunahakikisha vinakuwa na ubora unaotakiwa kabla havijatumika kwenye magari". Amesema Mhandisi Afrika.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages