Jumuiya ya wanafunzi watanzania katika Jamhuri ya watu wa China (TASAFIC) imefanikiwa kupata viongozi wapya ambao wataweza kuiongoza Jumuiya hiyo ambapo wateule hao wataongoza kwa kipindi cha mwaka mmoja 2024/25.
Uchaguzi huo ulifanyika Juni 30,2024 nchini China.
Akitangaza Majina ya washindi hao Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Stephen Bakari amesema waliochaguliwa ni Sabatho Jivitus, Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti Janeth Nyandiwa Mnyaga, Katibu Mkuu Chitalika Elieza Willium, Naibu Katibu Mkuu Paschal Anthony Jao na Mhazini ni Juliana Gaithan Kauno.
TASAFIC inafanya kazi kwa kushirikiana na ubalozi wa Tanzania nchini China kama walezi wa Shirikisho hilo.
Lengo la shirikisho hilo ni kuendeleza ushirikiano baina ya Wanafunzi na kuwaweka pamoja kama Watanzania.