Breaking

Thursday, 8 August 2024

CMSA:UWEKEZAJI MASOKO YA MITAJI WAONGEZEKA


Na Mwandishi wetu,Dodoma

MENEJA Uhusiano na Elimu kwa Umma wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Charles Shirima amesema uwekezaji katika kampuni za umma umeongezeka kwa kiwango cha juu tofauti na hapo awali.

Ameeleza hayo wakati akizungumza na wananchi pamoja na waandishi wa habari kwenye maonyesho ya nanenane kwa kubainisha kuwa wamekuja kutoa fursa kwa wananchi na wakulima wa kanda ya kati kujifunza kuhusu soko la mitaji na sekta ya soko la bidhaa ambalo wanaweza kuuza mazao kwa ushindani.

“CMSA kazi yetu ni kuratibu na kusimia shughuli za uendeshaji na usimamizi wa biashara katika soko la hisa na fursa za uwekezaji katika hisa za kampuni, hati fungani ambazo umma unaweza kuwekeza akiba kwa njia endelevu.

Mfumo huu pia unawezesha kampuni ni biashara mbalimbali ambapo serikali inaweza kukusanya mtaji kupitia umma unaowekeza katika Nyanja mbalimbali za uchumi wa mtu mmoja mmoja na umma.”

Alibainisha kuwa mwitikio ni mzuri na wawekezaji katika soko la mitaji ya umma wameongezeka kwa sana huku akitolea mfano kuwa ushiriki wa mifuko ya uwekezaji umekuwa mkubwa.

“Mwanzoni tulikuwa na mfuko mmoja tuu wa UTT-AMIS kwa sasa umeongezeka ushiriki katika hati fungani za serikali katika kampuni mwitikio umekuwa mkubwa.”

Kwa upande wake, Afisa Uhusiano na Elimu kwa umma CMSA, Stella Anastazi, alisema mamlaka hiyo imewezesha upatikanaji wa mitaji kwa kampuni na wameanzisha mfumo wa soko la bidhaa ili kutoa fursa kwa wakulima kupata masoko ndani na nje ya nchi.

Naye, Christopher Ngonyani kutoka CMSA, alisema uwekezaji huo umetoa fursa kwa watu kujipatia gawio na kuwepo ongezeko la thamani la uwekezaji wao huku akitoa rai kwa wananchi wasiowekeza kufanya hivyo.

“Moja ya changamoto ni ushiriki mdogo wa watanzania kuwekeza kwenye vipande hivyo tunatoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kuwekeza,”ameeleza.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages