Breaking

Monday 19 August 2024

ACHIMWENE SAFARI YAENDELEA KUJITOA KWA WAHITAJI GEREZA LA WANAWAKE SEGEREA




Kama tunavyoona taasisi, kampuni au makundi mbalimbali wakiwa na desturi ya kujitoa kwa jamii katika kutoa misaada ya kuwasaidia wahitaji wa aina mbalimbali.

Uongozi wa kampuni ya Achimwene Safari ikiongozwa na Meneja wake Ndugu Innocent Mbeyela wameendeleza desturi ya kuwasaidia wahitaji ambao akiwa pamoja na Wafanyakazi wa kampuni hiyo wakati wa zoezi la kutoa msaada kwa wafungwa wa Gereza la Wanawake Segerea mapema Agosti 17, 2024.

Akizungumza wakati wa zoezi la kuwatembelea na kuwakabidhi mahitaji mbalimbali, Meneja wa kampuni ya Achimwene Safari, Ndugu Innocent Mbeyela amesema kuwa wameona kufanya jambo hilo ni moja ya kupata baraka kupitia njia ya kujitoa kwao katika jamii zinazotunguka na pia kuonyesha umuhimu wa watu wenye uhitaji kuwa na wao wanapaswa kusaidiwa na kuthaminiwa.

"Achimwene Safari inaendelea na desturi hii ya kuwajali watu wenye uhitaji, ambapo awali tulitembelea gereza la mahabusu Segerea na leo tumetembelea gereza la wanawake ili kuona jinsi gani kila mtu ana umuhimu wa kuthaminiwa na kupata mahitaji muhimu kwa wakati sahihi," ameeleza.

Hata hivyo, Mkuu wa Gereza la Wanawake, Sp. Hamida Mussa Matimba ameishukuru kampuni ya Achimwene Safari kwa kuendelea kuwa na moyo huo wa kutoa msaada kwa wahitaji mbalimbali maana na wao wanahitajika kukumbukwa na kuthaminiwa kama watu wengine.

"Nipende kuwashukuru sana uongozi wa kampuni ya Achimwene Safari pamoja na wafanyakazi wake wote kwa desturi hii walioianzisha ya kutoa misaada kwa watu mbalimbali, Mungu azidi kuwabariki sana." ameeleza Sp. Matimba.

Kampuni ya Achimwene Safari ni moja ya kampuni za usafirishaji kwa kutumia mabasi ya njia ndefu hapa nchini yenye kufanya safari zake kila siku kutoka Dar es Salaam kuelekea Mbeya na pia kutoka Dar es Salaam kuelekea Chunya hadi Makongolosi.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages