Afisa Lishe Shirika la World Vision Tanzania Jane Mushi akitoa elimu kuhusu masuala ya lishe wakati wa maadhimisho ya wiki ya afya 'Afya Code Clinic' Mkoa wa Shinyanga
Meneja wa Mradi wa GROW ENRICH (Wilaya ya Kishapu na Shinyanga) kutoka World Vision Tanzania, Shukrani Dickson akitoa elimu kuhusu masuala ya lishe na afya wakati wa maadhimisho ya wiki ya afya 'Afya Code Clinic' Mkoa wa Shinyanga katika uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga Mjini
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Shirika la World Vision Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la KIVULINI limeshiriki Maadhimisho ya Wiki ya Afya ‘Afya Code Clinic’ Mkoa wa Shinyanga kwa kutoa elimu kwa wananchi kuhusu masuala ya lishe na afya na madhara ya ukatili wa kijinsia.
Maadhimisho ya Wiki ya Afya Mkoa wa Shinyanga yamefanyika katika uwanja wa CCM Kambarage Mjini S kuanzia Julai 24 – 27,2024 yakiratibiwa na Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na wadau wa afya.
Muonekano wa sehemu ya makundi 6 ya chakula ikiwamo nafaka, vyakula vya asili ya Wanyama, vyakula jamii ya mikunde, matunda, mbogamboga na kundi la sita ni sukari , asali na mafuta.
Meneja wa Mradi wa GROW ENRICH (Wilaya ya Kishapu na Shinyanga) kutoka World Vision Tanzania, Shukrani Dickson amesema wametumia maadhimisho hayo kutoa elimu kwa wananchi kuhusu masuala ya lishe na afya na kutetea haki na kupinga ukatili wa kijinsia.
“Sisi World Vision Tanzania tunafanya kazi katika wilaya ya Kishapu na Shinyanga tunashughulika na masuala ya lishe na afya na kutetea haki na kupinga ukatili wa kijinsia",amesema Shukrani.
Amesema katika Mkoa wa Shinyanga, Shirika la World Vision lina miradi katika wilaya za Shinyanga, Kishapu na Kahama likishirikiana na serikali na jamii kutoa huduma za jamii.
Ameitaja miradi hiyo kuwa ni Mpango wa Eneo Kilago uliopo Kahama, Mpango wa eneo Mwakipoya, Mpango wa eneo Lagana, Mradi wa NOURISH katika wilaya ya Kishapu na Mradi wa GROW ENRICH unaofanya kazi katika wilaya ya Kishapu na Shinyanga.
Shukrani amesema mradi wa GROW ENRICH unafadhiliwa na nchi ya Ujerumani na NOURISH unafadhiliwa na nchi ya Ireland na kwamba Miradi hiyo inafanya kazi ya kuboresha lishe, afya ya mama na mtoto, afya ya uzazi kwa vijana balehe katika wilaya za Kishapu na Shinyanga kwa kushirikiana na Shirika la KIVULINI.
Katika hatua nyingine, Shukrani ameeleza kuwa World Vision imejikita kufanya kazi na watoto, familia na jamii ili kupambana na umaskini na ukosefu wa haki limeendelea kuishirikisha jamii katika uboreshaji wa huduma kupitia miradi mbalimbali ya afya, lishe, elimu, uzalishaji mali na utetezi wa kijinsia ili kuhakikisha kuna ustawi wa mtoto.
Kwa upande wake Afisa Lishe Shirika la World Vision Tanzania Jane Mushi amesema wametoa elimu kwa jamii kuhusu masuala ya lishe baada ya kuona tatizo lililopo kwa mkoa wa Shinyanga kwamba chakula kipo lakini kuna ukosefu wa elimu kuhusu chakula gani wanatakiwa wale, wale vipi na kwa wakati gani.
“Mezani kwetu hapa tumeona baadhi ya vyakula kuwakilisha makundi 6 ya chakula ikiwamo nafaka, vyakula vya asili ya Wanyama, vyakula jamii ya mikunde, matunda, mbogamboga na kundi la sita ni sukari ,asali na mafuta , makundi haya sita yanatuletea mlo kamili”,amesema Mushi.
“Kwa hiyo tunahimiza wanajamii kutumia vyakula vinavyojumuisha makundi haya sita ya chakula ili kuhakikisha afya zetu zinakuwa bora na kupunguza tatizo la utapiamlo”,ameongeza Mushi.
Naye Jane Sologo kutoka Shirika la KIVULINI amesema wametumia maadhimisho hayo kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia kwa kuhamasisha jamii kuepukana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Meneja wa Mradi wa GROW ENRICH (Wilaya ya Kishapu na Shinyanga) kutoka World Vision Tanzania, Shukrani Dickson akitoa elimu kuhusu masuala ya lishe na afya wakati wa maadhimisho ya wiki ya afya 'Afya Code Clinic' Mkoa wa Shinyanga katika uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga Mjini- Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Afisa Lishe Shirika la World Vision Tanzania Jane Mushi akitoa elimu kuhusu masuala ya lishe wakati wa maadhimisho ya wiki ya afya 'Afya Code Clinic' Mkoa wa Shinyanga
Afisa Lishe Shirika la World Vision Tanzania Jane Mushi akitoa elimu kuhusu masuala ya lishe wakati wa maadhimisho ya wiki ya afya 'Afya Code Clinic' Mkoa wa Shinyanga
Afisa Lishe Shirika la World Vision Tanzania Jane Mushi akitoa elimu kuhusu masuala ya lishe wakati wa maadhimisho ya wiki ya afya 'Afya Code Clinic' Mkoa wa Shinyanga
Jane Sologo kutoka Shirika la KIVULINI akitoa elimu ya madhara ya ukatili wa kijinsia wakati wa maadhimisho ya wiki ya afya 'Afya Code Clinic' Mkoa wa Shinyanga

Elimu ya lishe na afya ikiendelea kutolewa wakati wa maadhimisho ya wiki ya afya 'Afya Code Clinic' Mkoa wa Shinyanga
Wafanyakazi wa Shirika la World Vision Tanzania na Shirika la KIVULINI wakiwa kwenye maadhimisho ya wiki ya afya 'Afya Code Clinic' Mkoa wa Shinyanga
Wafanyakazi wa Shirika la World Vision Tanzania na Shirika la KIVULINI wakiwa kwenye maadhimisho ya wiki ya afya 'Afya Code Clinic' Mkoa wa Shinyanga