Breaking

Friday 26 July 2024

WAZIRI NDEJEMBI ATAKA UADILIFU NA KUTENDA HAKI KWA WATUMISHI WA SEKTA YA ARDHI

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na viongozi pamoja na watumishi wa wizara ya Ardhi mkoa wa Dar es Salaam tarehe 26 Julai 2024 jijini Dar es Salaam.

Na Munir Shemweta, WANMM

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi amewataka watumishi wa sekta ya ardhi nchini kuongeza uadilifu na kutenda haki katika utekelezaji wa majukumu yao sambamba na kuongeza kasi katika utendaji kazi.

Mhe. Ndejembi namesema, suala la ardhi ni gumu na linahitaji watumishi kuwa makini ambapo amesisitiza kuwa ni lazima watumishi wa sekta ya ardhi watende haki huku wakizingatia kuwa kuna sheria, kanuni na miongozo inayowaoongoza katika utendaji kazi.

Aidha, Mhe. Ndejembi amesema, yale yote mazuri yaliyofanywa na mtangulizi wake ikiwemo Klinik za Ardhi atayaendendeleza kwa lengo la kuleta ufanisi wa wizara.

‘’Sikuja kutengua torati, yote aliyoyaanzisha mtanguluzi wangu ikiwemo klinik za ardhi zitaendelea na vile vile anayehisi jambo lake limekwama ajitokeze na atahudumiwa’’ amesema Mhe. Ndejembi.

Mhe. Ndejembi ametoa kauli hiyo tarehe 26 Julai 2024 wakati akizungumza na viongozi pamoja na watumishi wa Wizara ya Ardhi mkoa wa Dar es Salaam mara baada ya kutoka kuapishwa kushika nafasi hiyo kutoka kwa mtangulizi wake Mhe. Jerry Silaa.

Sambamba na hayo Waziri huyo wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ametaka kuimarishwa kwa mifumo ndani ya wizara ili migogoro ya ardhi isiendelee kujitokeza.

Mhe. Ndejembi ameapishwa na Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi akitokea Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Watu wenye ulemavu).

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akizungumza mara baada ya kuwasili kwa waziri wa wizara hiyo Mhe. Deogratoius Ndejembi kwenye ofisi za wizara Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Mhandisi Anthony Sanga akizungumza mara baada ya kuwasili kwa waziri wa wizara hiyo Mhe. Deogratoius Ndejembi katika ofisi za wizara Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Lucy Kabyemera, Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Hamad Abdallah na Kamishna wa Ardhi nchini Nathaniel Nhonge wakimsikiliza Waziri wa Ardhi Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) alipowasili kwa mara ya kwanza katika ofisi za ardhi Dar es Salaam tarehe 26 Julai 2024.
Sehemu ya watumishi wa wizara ya Ardhi.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na Naibu waziri wake Mhe. Geophrey Pinda (kushoto) pamoja na Katibu Mkuu Mhandisi Anthony Sanga (kulia) alipowasili ofisi za ardhi Dar es Salaam mara baada ya kutoka kuapishwa tarehe 26 Julai 2024 jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na Naibu waziri wake Mhe. Geophrey Pinda (kushoto), Katibu Mkuu Mhandisi Anthony Sanga (wa pili kulia) pamoja na Naibu Katibu Mkuu Lucy Kabyemera alipowasili ofisi za ardhi Dar es Salaam mara baada ya kutoka kuapishwa  tarehe 26 Julai 2024 jijini Dar es Salaam.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages