Breaking

Tuesday 2 July 2024

WAZIRI AWESO AFURAHISHWA HUDUMA KWA WATEJA DAWASA

Waziri wa Maji Jumaa Aweso amefurahishwa na kauli njema kutoka mmoja wa wahudumu kwa wateja wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) wakati wa ziara yake inayoendelea Jijini Dar es salaam alipopiga namba hiyo 0800110064 inayopatikana bila malipo na kuongea na mhudumu kwa weledi zaidi kwa kuhakikishiwa huduma bila usumbufu.

Amefanya zoezi hilo akiwa katika Mtaa wa Kibululu Kata ya Goba Wilayani Ubungo alipokutana na Wananchi wakati wa kusikiliza changamoto za huduma ya Maji.







Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages