Breaking

Monday, 1 July 2024

UBORESHAJI HUDUMA YA MAJI MAKABE



Zoezi la kuongeza msukumo wa maji kwa wakazi wa maeneo ya Makabe Nyota njema, Makabe Dubai na Ubata Kata ya Mbezi linaendelea kutelekezwa na mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA).

Zoezi hilo limehusisha utoaji wa toleo kwenye bomba la inchi 10 kwa umbali wa mita 1000 kwenda kujazia maji kwenye bomba la inchi 6 , inchi 4 na bomba la inchi 3 yanayohudumia maeneo hayo.

Kukamilika kwa zoezi hilo kutanufaisha wakazi zaidi ya 200 wa maeneo tajwa, Mamlaka inaendelea na jitihada za kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma ya majisafi na ya kutosheleza.





Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages