Breaking

Tuesday 16 July 2024

RHMT’s & CHMT’s LINDI WATAKIWA KUSHIRIKIANA

Kaimu Katibu Tawala wa mkoa wa LIndi Natalis Linuma amezitaka Timu za Usimamizi wa Shughuli za Afya za Halmashauri (CHMT’s) na mkoa (RHM) za mkoa wa Lindi kuwa na ushirikiano katika kutekeleza majukumu ya usimaizi katika huduma za Afya na kila moja awajibike katika eneo lake ili kuboresha huduma katika maeneo ya kutolea huduma za Afya.

Linuma ametoa maelekezo hayo wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara ya Timu ya Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe kutoka Ofisi ya Rais- TAMISEMI,Timu za Usimamizi wa Shughuli za Afya za Halmashauri(CHMT) na mkoa (RHMT) baada ya kukamilisha ziara ya usimamizi shirikishi na ufuatiliaji wa huduma za Afya katika mkoa wa Lindi.

“Ni vizuri tukafanya kazi kama timu na timu hizi zinatofautiana kuwa kuna nyingine ya wilaya na nyingine ya mkoa kwahiyo kwenye timu siku zote jambo haliharibiki na tunatakiwa kuwa na umoja katika kutekeleza majukumu na kila mtu kwenye eneo lake ahakikishe jukumu analopewa analisimamia ipasavyo na linakamilishwa kwa ukamilifu na uadilifu mkubwa” amesema

Akisisitiza hilo kwa Niaba ya Ofisi ya Rais - TAMISEMI Dkt. Rashid Mfaume,Mkurugenzi wa Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe amesema katika maeneo mengi waliyopita timu hizo zimekuwa hazifanyi kazi ya usimamizi shirikishi na wajumbe wa timu hizo wamekuwa hawawajibiki katika maeneo yao.

“Bahati mbaya tumekuwa tukiwapima kwa vituo ambavyo mmevitembelea tumegundua hamuangalii quality (ubora) na kipimo cha ubora kwa namna ya tulivyotembelea tungekuta changamoto ni chache sana kuliko ambavyo mmeona kwahiyo tunachangamoto ya ubora kwa hizi ‘Supportive Supervision’ na maelekezo yetu sisi ni kuwa tumekuja kuonesha njia na mnaona timu ilivyokuwa kubwa hatujigawi katika vikundi vidogo nendeni kama timu mkofika Hospitalini mjigawe na kila swali unalouliza ukiambiwa ndio thibitisha” amesema Dkt. Mfaume.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages