Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Kenan Kihongosi amechangia kiasi Cha Shilingi laki Tano kwa ajili ya shughuli mbalimbali za Maendeleo katika Kijiji cha Ngwaunkwaya Kata ya Banemi Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi.
Mhe.Kihongosi ametoa Fedha hizo huo baada ya kufurahishwa na mwamko wa Kijiji hicho katika kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo.
Mhe.Kihongosi yupo katika ziara ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za Wananchi Mkoani Simiyu ikiwa ni Siku kadhaa tangu kuripoti katika Kituo chake kipya cha kazi tangu alipoteuliwa na Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu kushika wadhfa wa ukuu wa Mkoa wa Simiyu .
SIMIYU RS
03 Julai 2024.