Breaking

Monday 1 July 2024

RC KIHONGOSI AAGIZA KUPATIKANA UMEME, MAJI NDANI YA MIEZI 3 SHULE YA SEKONDARI MWABUMA

Mkuu wa Mkoa Simiyu Mhe.Kenan Laban Kihongosi ameagiza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu ndani ya miezi mitatu kuhakikisha huduma ya Maji na Umeme vinapatikana katika Shule ya Sekondari Mwabuma.

Mhe.Kihongosi ametoa agizo hilo alipokuwa akisikiliza kero za Wananchi katika Kata ya Mwabuma Wilayani Meatu katika ziara yake ya ukaguzi wa Miradi,kusikiliza na kitatua Kero za Wananchi.

Aidha amemuagiza uongozi Wilayani Meatu kuhakikisha Wanasimamia kwa karibu utatuzi wa changamoto ya Maji na Umeme katika Kata ya Mwabuma kiujumla

Wananchi wa Mwabuma wamemueleza Mkuu wa Mkoa Kihongosi kuwa kukosekana kwa umeme na Maji katika Shule ya Sekondari Mwabuma kumeathiri kwa kiasi kikubwa Wanafunzi kimasomo.

Mkuu wa Mkoa Kihongosi yuko katika ziara Wilayani Meatu kwa ajili ya ukaguzi wa Miradi na kusikiliza kero mbalimbali za Wananchi.


SIMIYU-RS

01 Julai 2024.






Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages