Breaking

Monday, 8 July 2024

MSIMU WA SABASABA, TFS YATOA OFA KWA WATALII

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wametoa ofa ya kutembelea vivutio Vya utalii ikolojia kwenye hifadhi ya msitu wa Mazingira asilia Pugu Kazimzumbwi na Vikindu Pamoja vivutio vya historia vilivyopo Bagamoyo katika kipindi hiki cha msimu wa Sabasaba.

Akizungumza na Wanadishi wa habari leo Julai 8,2024 Pugu Jijini Dar es Salaam, Afisa Utalii, Mbarouk Sinon amesema ofa hiyo imeanza June 28,2024 ambapo itamalizika Julai 13,2024.

Amesema ofa hiyo inapatikana kwa wananchi watakaotembelea TFS katika banda la Maliasili na Utalii kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa sabasaba yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.

Sinon amesema mpaka sasa watalii wameshapata ofa hiyo na kuweza kutembelea vivuti katika maeneo hayo kwa kipindi hiki cha Sabasaba.

“Watalii mbalimbali wameshaanza kutumia fursa hii, na leo kuna watalii kutoka nje ya nchi pamoja na watalii kutoka katika mikoa mbalimbali hapa nchi wametembelea hifadhi ya Mazingira asili Pugu Kazimzumbwi na kujionea vivutio kadhaa”. Amesema Sinon.

Pamoja na hayo amewakaribisha wananchi kutembelea banda la Maliasili na Utalii kwenye Maonesho sabasaba ili waweze kupata ofa hiyo.

Kwa upande wake Mtalii (mtanzania) Jadida Athumani amesema amefurahia ofa hiyo kwani amepata fursa ya kutemebelea vivutio kama hifadhi ya Mazingira asili Pugu Kazimzumbi ambapo ameendesha mtumbwi kwenye hifadhi hiyo na pia kujionea vivutio mbalimbali ambavyo vipo kwenye hifadhi hiyo.

"Naipongeza TFS kwa kutoa ofa hii ambayo imenifanya miweze kutembelea hifadhi hii ya Mazingira ya asili Pugu Kazimzumbwi na kujionea vivutio mbalimbali vya kuvutia, nawaomba watanzania wenzangu  kutembelea banda la Maliasili na Utalii ili waweze kupata ofa hii.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages