Breaking

Tuesday 2 July 2024

KITUO CHA AFYA CHA GUMANGA CHAFANYA UPASUAJI MKUBWA WA KWANZA


Kituo cha Afya  cha Gumanga kilichopo kata ya Gumanga Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama kimefanikiwa kufanya upasuajia mkubwa wa kwanza wa dharura kwa mama mjamzito  toka kufunguliwa kwake.

Akizungumza mara baada ya upasuaji huo, Mganga Mkuu wilaya ya Mkalama Dkt. Solomon Michael amesema upasuaji huo umefanyika Julai 01,2024 chini ya  madaktari wawili wakisaidiwa na wauguzi pamoja na mtalaamu wa usingizi.

"Kwa mara ya kwanza tumefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa hapa Gumanga toka tuanzishe huduma hizi za upasuaji. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu. Mtoto aliyezaliwa ni wa kike na uzito wa kilo 3.1, hali  ya mama na mtoto inaendelea vizuri" aliongeza Dkt. Michael. 
Kwa mujibu wa Dkt. Solomon Michael amesema mjamzito huyo amefika kituoni hapo siku ya Jumatatu ya Julai 1,2024 muda wa asubuhi na kufanyiwa upasuaji muda wa saa moja usiku. 

Aidha timu ya wataalamu iliyoongoza zoezi hilo ni Dkt. Sira Laurent Kisamhara, akisaidiwa na Dkt. Lazaro Chambo, wauguzi wakiwa Seleman Mwalukasa, Faraja Shadrack, na Richard Sopeter mtaalamu wa usingzi pamoja a mtaalam wa Maabara Patric Sanga

Kituo cha afya cha Gumanga kinakuwa ni kituo cha tatu cha serikali wilayani Mkalama kinachotoa huduma za upasuaji, vingine ni Hosipitali ya Wilaya ya Mkalama pamoja na  kituo cha Afya cha Kinyambuli.

 

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages