Breaking

Tuesday 9 July 2024

DAWASA YATEKELEZA AGIZO LA WAZIRI AWESO KIGAMBONI



Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) imeanza utekelezaji wa agizo la Waziri wa Maji Mh.Jumaa Aweso (Mb) la kufanya maunganisho ya Majisafi kwa wananchi wa maeneo ya Kigamboni kwa kutoa vifaa vya maunganisho ya majisafi kwa wakazi 45 waliokwisha lipia kupata huduma hiyo.

Akizungumza katika makabidhiano ya vifaa hivyo, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA, Mhandisi Mkama Bwire amewahamasisha wananchi takribani 400 waliokwisha pokea makisio ya gharama za kuungiwa maji kulipia kwa wakati Ili waweze kuungiwa huduma hiyo, huku akiwataka wale ambao bado hawajapeleka maombi ya kupatiwa huduma kufanya hivyo Ili waweze kufanyiwa upimaji na kunufaika na huduma ya majisafi.

Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kigamboni, Ndugu Stanley Mkandawile ameishukuru Serikali kupitia DAWASA kwa kuitikia kilio cha wananchi kuhusu huduma ya maji kwa kutoa vifaa vya kuwaunganisha wateja na majisafi, na kutoa wito kwa waliopata makisio ya gharama za kuungiwa maji kulipia mapema Ili waweze kupata huduma hiyo.

Naye mmoja wa wanufaika wa zoezi la maunganisho mapya Ndugu Yusufu Msabila anaishukuru Mamlaka kwa kumfungia maji nyumbani kwake na sasa anaanza kunufaika na huduma.



Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages