Breaking

Wednesday 31 July 2024

DAWASA KUUNGANISHA HUDUMA YA MAJISAFI WATEJA ZAIDI YA 200 TEGETA



Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) imeendelea na zoezi la ugawaji wa vifaa vya maunganisho mapya kwa wateja zaidi ya 200 katika mitaa mbalimbali ya Tegeta ikiwemo Wazo, Salasala, Kunduchi, Mbweni na Boko walioomba na kulipia kupata huduma hiyo.

Akizungumza zoezi hilo Meneja wa Mkoa wa kihuduma DAWASA - Tegeta ndugu, Victoria Masele amewashukuru wateja wote kwakua wavumilivu mpaka muda huu ambao sasa wanaenda kuungwa na huduma ya majisafi.

"Niwashukuru wateja kwakuvumilia kipindi chote walipokua wakisubiri kupatiwa vifaa hivi, wateja hawa 200 wote tunaenda kuwaunga na huduma ya majisafi kwa kipindi kifupi sana Ili waanze kufurahia huduma kutoka DAWASA" ameeleza ndugu, Masele.

Ndugu Masele ametoa wito kwa wananchi ambao waliofanya maombi na wamekwishapatiwa kumbukumbu namba kwajili ya kufanya malipo basi waweze kukamilisha zoezi la ulipaji Ili na wao wapate huduma.

Kwa upande wake ndugu, Hillary Kimambo mkazi wa Mbweni ameishukuru DAWASA kwakuwapatia vifaa hivi kwani wanaenda kupata huduma ya majisafi na kuondokana na changamoto ya kununua maji kwa gharama kubwa huku muda mwingi wakiwa hawana uhakika na usalama wa maji hayo Kitendo ambacho kilihatarisha afya zao.






Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages