Breaking

Sunday, 21 July 2024

BENDERA YA MICHEZO TPDC, YAPEPERUSHWA VYEMA

  


Kikosi cha TPDC

Mapema asubuhi ya leo Julai 21, 2024 timu ya mpira wa miguu ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)  imecheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Tanga All stars katika uwanja wa Mikocheni-TPDC.

Mchezo huo uliokuwa wa kasi na wakuvutia kwa pande zote mbili umemalizika kwa TPDC kuvuna point tatu Kwa ushindi wa bao 5:3.Waliocheka na nyavu ni mshambualiaji Donald Aponde 43°, Ismail Naleja 55°, Dalushi Shija 65, Isack Mtei 75° na George Leonard 89°.

Ikumbukwe kuwa michezo hii ya kirafiki ni sehemu ya mazoezi Kwa timu ya TPDC kuelekea  mashindano ya SHIMMUTA yatakayofanyika Novemba, 2024 jijini Tanga.

Kocha wa timu ya TPDC  Mwalimu Bizoo Bituka amesema kuwa ameridhishwa na maandalizi ya kikosi  na kikosi kipo tayari kwenda kupeperusha vyema bendera ya TPDC katika mashindano ya SHIMMUTA.

''Mpaka sasa Maendeleo ya  timu ya TPDC ni mazuri kwani hadi sasa  tumecheza michezo ya kirafiki mitano (5)  na hatujapoteza mchezo wowote'', aliongea Kocha Bizoo.

1.TPDC 4  VS 1MRC

2.TPDC 3 VS 1 DIT

3.TPDC 3 VS 1Mkemia Mkuu

4.TPDC 5 VS 1 Umoja Veteran

5.TPDC 5 VS 3 Tanga All stars

    #TPDCTUNAWEZESHA

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages