Breaking

Tuesday 16 July 2024

ATCL NA HOSPITALI YA KOKILABEN WATOA OFA YA UPIMAJI AFYA INDIA KWA GHARAMA NAFUU

KAMPUNI ya ndege ya Tanzania (ATCL), imeanzisha kampeni ya miezi mitatu  ya “Afya yangu maisha yangu” ikiwa na lengo la kuhamasisha wananchi wa Tanzania, Kenya na Uganda kujali afya zao.

Kampeni hiyo ilianza Julai 15 na itamazilika mwezi Oktoba mwishoni na inaendeshwa kwa ushirikiano kati ya ATCL na hospitali kubwa ya India ya Kokilaben ambapo watu watakwenda kufanya kipimo kikubwa cha afya kwa gharama nafuu.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam wakati akiitambulisha kampeni hiyo Kampeni hiyo, Mkurugenzi wa Biashara wa ATCL Bw. Patrick Ndekana alisema mpango huo unasisitiza kujitolea kwa ATCL katika kutangaza suluhisho la afya kwa ujumla na kuongeza uzoefu wa usafiri kwa wateja wote.

"Ninafuraha kutangaza mpango wa kusisimua unaoonyesha dhamira ya Air Tanzania kwa ustawi na ustawi wa wasafiri na wadau wetu. Tangu Agosti 2023, Air Tanzania imeanzisha ushirikiano wa kibiashara na Hospitali ya Kokilaben iliyopo Mumbai lengo ni kusaidia watanzania kupima afya zao," alisema.

Ndekana amesema ushirikiano huo unawawezesha abiria wanaotumia ndege za ATCL safari tano za kila wiki kwenda Mumbai, kunufaika na punguzo la gharama za matibabu wanapokwenda kupata matibabu hospitalini hapo.

Amesema kwa muda wa miezi mitatu ijayo, kuanzia leo Julai 16, 2024 hadi Oktoba 16, 2024, Hospitali ya Kokilaben itatoa huduma za afya kwa punguzo la bei kwa kushirikiana na Air Tanzania pamoja na vipimo vingine vya hali ya juu ikiwemo PET-CT scan.

Aidha ameongeza kuwa uchunguzi wa PET unajulikana kwa usahihi wake katika kutambua mapema hali ya matibabu, kuwawezesha abiria wa ATCL kufahamu umuhimu wa afya zao.

Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na David Dickson ambaye ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mumbai Healthcare Services ambaye amewaomba watanzania kujitokeza kwa wingi kutumia fursa hiyo ya kukagua afya zao.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages