Breaking

Thursday 27 June 2024

WATU 23 WAFARIKI, 336 WAJERUHIWA MAANDAMANO KENYA



Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu ya Kenya (KNCHR) imetoa ripoti ya kina kuhusu idadi ya vifo wakati wa maandamano ya kupinga Mswada wa Fedha wa 2024.

Katika taarifa ya Jumatano, Juni 26, KNCHR ilikashifu Huduma ya Kitaifa ya Polisi kwa kutumia nguvu kupita kiasi kwa waandamanaji.

KNCHR ilidokeza kuwa uchunguzi wake ulionyesha kuwa Wakenya 21 waliuawa kwa kutumia risasi za moto katika maeneo mbalimbali nchini.

"Tume kufikia sasa imerekodi vifo 21 vya watu waliopigwa risasi wakati wa maandamano. Ripoti zinaonyesha kuwa wengi wa waliofariki walipigwa risasi za moto wakati wa maandamano," KNCHR ilisema.

Tume hizo ya haki za binadamu zimeongeza kuwa waandamanaji 336 na maafisa wa polisi walipata majeraha mbalimbali wakati wa maandamano hayo.

Kulingana na KNCHR, majeraha hayo yalikuwa ya kuvunjika, majeraha ya risasi na kuvuta hewa ya vitoa machozi.

"Tume imerekodi waandamanaji 336 na askari polisi waliojeruhiwa tangu kuanza kwa maandamano hayo Juni 18. Majeruhi hao ni kati ya kuvunjika, majeraha ya risasi, majeraha ya tishu laini na kuvuta gesi ya machozi. Waliojeruhiwa vibaya walipelekwa hospitali kwa matibabu maalumu,” waliongeza.

Tume hiyo pia ilifichua kuwa watu 22 wametekwa nyara na asasi za usalama kwa kuhusishwa na maandamano ya kupinga Mswada wa Fedha wa 2024.

“Tume inafahamu kuwa kufikia sasa, watu 22 wametekwa nyara na 53 kukamatwa kiholela, wakiwemo madaktari na mawakili,” KNCHR iliongeza.




Source : Tuko News
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages