NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
CHUO Kikuu cha Dar es Salaam kimetakiwa kupanua wigo wa wiki ya utafiti na ubunifu kwa kushirikisha washirika wa utafiti ambao tafiti zao zimesajiliwa na zina uhusiano na idara mbalimbali za kitaaluma.
Wito huo umetolewa leo Juni 07, 2024, Jijini Dar es Sslaam, na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Franklin Rwezimula katika hafla ya kuhitimisha maadhimisho ya 9 ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
Akizungumza katika hafla hiyo, Dkt. Rwezimula amesema ni vyema maadhimisho hayo yakawa yanafanyika kama sehemu ya matukio ya kuelekea Maadhimisho ya Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu, ambayo yatakuwa yanafanyika kati ya tarehe 27 hadi 31 Mei, kila mwaka.
Matokeo ya tafiti zinazofanywa na vyuo mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yamekuwa ni rejea muhimu katika utekelezaji wa sera, mipango na mikakati mbalimbali ya kitaifa, kikanda na kimataifa katika masuala ya utafiti na ubunifu.
"Maadhimisho haya yanatoa jukwaa zuri la kuhamasisha kizazi cha wanataaluma wachanga na chipukizi kufanya utafiti na ubunifu unaojibu changamoto za kiuchumi na kijamii katika nchi yetu na dunia kwa ujumla". Amesema
Amesema ikiwa vyuo vikuu nchini Tanzania vitaonesha kwa umma kazi zao za kitaaluma na zinazotokana na matokeo ya utafiti, vitaishawishi serikali na soko la ajira, kuboresha uhusiano uliopo baina ya vyuo vikuu na waajiri na wafadhili na hatimaye kutoa fursa ya ushirikiano ndani na nje ya nchi.
Kwa upande wake Kaimu Naibu Makamu Mkuu Wa Chuo – Utafiti, Prof. Nelson Boniface amesema maadhimisho hayo yalihusisha wafanyakazi na wanafunzi kushiriki kuonesha shughuli na miradi yao mbalimbali ya utafiti na ubunifu katika ngazi husika.
"Katika ngazi ya Vitengo, jumla ya miradi 306 ilionyeshwa ambayo ilikuwa katika maeneo (categories) makundi tisa (9). Kati ya kazi hizo, kazi 205 (67%) zilionyeshwa na wafanyakazi na wanafunzi wanaume huku kazi 101 (33%) zilionyeshwa na wafanyakazi na wanafunzi wanawake". Amesema Prof. Boniface
Pamoja na hayo amesema kati ya kazi 306 za mwaka huu, kazi za wafanyakazi zilikuwa 82 (27%) na za wanafunzi zilikuwa 224 (77%). "Hii inaonesha ni kiasi gani Chuo chetu kimejikita katika kuhamasisha wanafunzi wetu kuwa sehemu ya watafiti na wabunifu na kuwajengea uwezo kuwa chachu ya maendeleo ya nchi yetu".
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Franklin Rwezimula akizungumza katika hafla ya kuhitimisha maadhimisho ya 9 ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam leo Juni 07, 2024, Jijini Dar es Sslaam
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Franklin Rwezimula akizungumza katika hafla ya kuhitimisha maadhimisho ya 9 ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam leo Juni 07, 2024, Jijini Dar es Sslaam
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Franklin Rwezimula akizungumza katika hafla ya kuhitimisha maadhimisho ya 9 ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam leo Juni 07, 2024, Jijini Dar es Sslaam.
Kaimu Naibu Makamu Mkuu Wa Chuo – Utafiti, Prof. Nelson Boniface akizungumza katika hafla ya kuhitimisha maadhimisho ya 9 ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam leo Juni 07, 2024, Jijini Dar es Sslaam.
Baadh ya wadau wakiwa katika hafla ya kuhitimisha maadhimisho ya 9 ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam leo Juni 07, 2024, Jijini Dar es Sslaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)