Breaking

Tuesday, 18 June 2024

THPS YATOA ELIMU HUDUMA ZA AFYA ZINAZOTOLEWA KUPITIA MRADI WA CDC/PEPFAR AFYA HATUA

Mkurugenzi wa Huduma za Jamii wa Shirika la THPS, Dkt. Appolinary Bukuku akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha siku mbili kati ya THPS na Wahariri na Waandishi wa Habari kilichofanyika Jijini Tanga.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Shirika la Tanzania Health Promotion Support (THPS) linalotekeleza afua mbalimbali za afya nchini kupitia mradi wa Afya Hatua kwa ufadhili wa Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na UKIMWI (PEPFAR) kupitia Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Marekani (U.S. CDC) limefanya Kikao Kazi na Wahariri na Waandishi wa Habari ili kuimarisha ushirikiano kati ya THPS na waandishi wa habari katika kuhabarisha na kuelimisha jamii juu ya huduma mbalimbali za afya.

Kikao kazi hicho cha siku mbili (Juni 18 na 19 ,2024) kilichoshirikisha waandishi wa habari na wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini Tanzania kimefunguliwa Jijini Tanga na Mkurugenzi wa Huduma za Jamii wa Shirika la THPS, Dkt. Appolinary Bukuku.

Akizungumza wakati wa kikao hicho, Dkt. Bukuku amesema Waandishi wa habari ni kundi muhimu sana katika jamii linalopaswa kupata taarifa sahihi za afya ili kuweza kuhabarisha na kuelimisha jamii.

Waandishi wa habari mkipata taarifa iliyo sahihi itasaidia kupunguza taharuki katika masuala ya afya nchini.Tunapenda mkipata taarifa sahihi inakuwa rahisi kuiambia jamii kuhusu taarifa sahihi ili kuepusha taharuki katika jamii zinapotokea taarifa zisizo sahihi”,amesema Dkt. Bukuku.

Tunaamini tukiwa tunapata taarifa sahihi kutoka kwa sauti ya jamii (Waandishi wa habari), tutaifikia jamii kwa urahisi na elimu hiyo ya afya itakuwa sahihi. Na kutokana na kutambua hilo ndiyo maana timu ya Mawasiliano kutoka THPS imeandaa kikao hiki ili tukae pamoja, tuongee, tupeane taarifa za afya, tujue THPS inafanya nini hapa nchini kwenye jamii.

“Tunaamini nyinyi mnaweza kuwa chumvi katika tasnia ya habari na kuwajulisha wengine kuhusu nini kinafanyika kwenye miradi ya afya inayotekelezwa na THPS. THPS pia inawakilisha mashirika mengine yanayofanya kazi kama zetu, kwa hiyo kupitia sisi mnaweza kujifunza vitu vingi vinavyofanyika kwenye Programu za afya kupitia ufadhili wa PEPFAR kupitia U.S. CDC”,ameongeza.

Dkt. Bukuku ameeleza kuwa miongoni mwa miradi inayotekelezwa na THPS ni Mradi wa Afya Hatua unaofadhiliwa na PEPFAR kupitia U.S. CDC katika mikoa ya Tanga, Shinyanga, Pwani na Kigoma.

Kwa upande wake, Meneja Mawasiliano THPS, Henry Mazunda amevipongeza na kuvishukuru vyombo vya habari kwa mchango wake Shirika la THPS katika kuhabarisha umma kuhusu masuala ya afya huku akiomba habari zinazohusu afya zipewe kipaumbele.

Tunapenda kuona ukaribu uliopo baina ya THPS na Waandishi wa habari uendelea kuimarika zaidi ili kuhakikisha jamii inapata taarifa sahihi na kufanya maamuzi sahihi kuhusu masuala ya afya. Kikao kazi hiki kinalenga kuweka ukaribu zaidi uhusiano wetu THPS na waandishi wa habari.

THPS imekuwa ikishirikiana na waandishi wa habari katika utekelezaji wa shughuli zake mbalimbali. Kwa mfano, tumekuwa tukiandaa ziara za waandishi wa habari kutembelea maeneo mbalimbali ambako tunatekeleza shughuli za miradi yetu. Pia tumekuwa tukiwaalika waandishi kushiriki matukio yet una tutaendelea kufanya hivyo”,amesema Mazunda.

Nao washiriki wa kikao hicho wameishukuru THPS kwa kuwajengea uwezo wahariri na waandishi wa habari kuhusu masuala ya afya na kuiomba kuendelea kuwafikia waandishi wa habari wengi zaidi kwenye maeneo wanayotekeleza miradi ili kuiwezesha jamii kupata taarifa sahihi kuhusu masuala ya afya.

Mradi wa Afya Hatua unalenga kutoa huduma jumuishi katika vituo vya afya katika mikoa ya Kigoma, Pwani, Shinyanga na Tanga) na katika jamii (Kigoma, Pwani na Tanga. 

Huduma hizi ni pamoja na matibabu na matunzo ya watu wanaoishi na VVU, huduma za kitabibu za tohara kinga kwa wanaume, kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, pamoja na afua zingine.
Mkurugenzi wa Huduma za Jamii wa Shirika la THPS, Dkt. Appolinary Bukuku akizungumza leo Jumanne Juni 18,2024 katika ukumbi wa YDCP Jijini Tanga wakati akifungua kikao kazi cha siku mbili kati ya THPS na Wahariri na Waandishi wa Habari - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi wa Huduma za Jamii wa Shirika la THPS, Dkt. Appolinary Bukuku akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha siku mbili kati ya THPS na Wahariri na Waandishi wa Habari kilichofanyika Jijini Tanga.
Mkurugenzi wa Huduma za Jamii wa Shirika la THPS, Dkt. Appolinary Bukuku akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha siku mbili kati ya THPS na Wahariri na Waandishi wa Habari kilichofanyika Jijini Tanga.
Mkurugenzi wa Huduma za Jamii wa Shirika la THPS, Dkt. Appolinary Bukuku akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha siku mbili kati ya THPS na Wahariri na Waandishi wa Habari kilichofanyika Jijini Tanga.
Mkurugenzi wa Huduma za Jamii wa Shirika la THPS, Dkt. Appolinary Bukuku akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha siku mbili kati ya THPS na Wahariri na Waandishi wa Habari kilichofanyika Jijini Tanga.
 Wahariri na Waandishi wa Habari wakiwa kwenye kikao kazi chao na THPS 

Kikao kazi baina ya Wahariri na Waandishi wa Habari na THPS kikiendelea

Meneja Mawasiliano THPS, Henry Mazunda akizungumza wakati wa kikao kazi kati ya THPS na Wahariri na Waandishi wa Habari kilichofanyika Jijini Tanga.

Meneja Mawasiliano THPS, Henry Mazunda na Afisa Mawasiliano THPS Mercy Nyanda (kulia) wakiteta jambo kikao kazi kati ya THPS na Wahariri na Waandishi wa Habari kilichofanyika Jijini Tanga.
Afisa Mawasiliano THPS Mercy Nyanda akizungumza wakati wa kikao kazi kati ya THPS na Wahariri na Waandishi wa Habari kilichofanyika Jijini Tanga.

Meneja wa Mradi wa THPS Afya Hatua wa Mkoa wa Tanga Dkt. Otmar Massawa akizungumza wakati wa kikao kazi kati ya THPS na Wahariri na Waandishi wa Habari kilichofanyika Jijini Tanga.

Mshauri wa Mradi wa Afya Hatua kwenye Huduma za Kinga kutoka THPS Japhet Daud akizungumza wakati wa kikao kazi kati ya THPS na Wahariri na Waandishi wa Habari kilichofanyika Jijini Tanga.

Mhariri Lilian Timbuka akichangia hoja wakati wa Kikao kazi baina ya Wahariri na Waandishi wa Habari na THPS

Picha ya pamoja Wahariri na Waandishi wa Habari na wafanyakazi wa THPS
Picha ya pamoja Wahariri na Waandishi wa Habari na wafanyakazi wa THPS.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages