Breaking

Sunday 30 June 2024

SEVERINE MBULLU ATEULIWA KUGOMBEA UENYEKITI UVCCM SHINYANGA



Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa (NEC) imefanya uteuzi wa Wanachama watakaogombea nafasi wazi za uongozi katika Chama na Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM).

Katika uteuzi huo kamati imemteua Ndugu Severine Leonard Mbullu kugombea nafasi ya Mwenyekiti Wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga.


Uteuzi huo umefanywa katika kikao chake cha kawaida leo tarehe 30 Juni, 2024 jijini Dar Es Salaam chini ya Mwenyekiti wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Taanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages