Breaking

Sunday 23 June 2024

RC CHALAMILA ATAKA WAFANYABIARA KUTOJIHUSISHA NA MIGOMO



Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila amewataka wafanyabiasha kutojihusisha na mgomo. 

Rc Chalamila ameyasema hayo mapema leo Juni 23,2024 Kufuatia uwepo wa taarifa za uvumi wa mgomo wa wafanyabiashara wa kariakoo. 

RC Chalamila amewataka wafanyabiashara kuepuka kushiriki kwenye masuala yanayoweza kuleta uvunjifu wa amani na kurudisha nyuma uchumi ikiwemo mgomo huu. 

Amesema Serikali imeshashughulikia baadhi ya changamoto na inaendelea kushughulikia changamoto za wafanyabiashara hususani zile zinazohusu mabadiliko ya Kisheria.

RC Chalamila amewataka wafanyabiashara kutambua kuwa mgomo sio suluhisho pekee la kutatua changamoto bali utaratibu bora wa kutatua changamoto ni kukaa mezani na mamlaka kujadili kwani mgomo huongeza chuki na wakati mwingine kusababisha uvunjifu wa amani.

Aidha amesema Serikali inatambua changamoto za wafanyabiashara na kada zingine za wafanyakazi na watumishi na inaendelea kuzifanyia kazi hivyo amewataka wafanyabiashara kushirikiana na Serikali kumaliza changamoto zao na kuepuka mihemko inayoanzishwa na watu wachache wasio kuwa na nia njema na Mkoa wa Dar es salaam na Taifa kwa ujumla.

Sanjari na hilo RC Chalamila amesema ujenzi wa soko jipya la kariakoo na ukarabati wa soko liloloungua kuwa soko hilo linalojengwa kwa zaidi ya shilingi bilioni 28 lipo katika hatua za mwisho na kwamba Rais Dokta Samia atakuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa soko hilo na wafanyabiashara waliokuwepo zamani na wapya wataingia kwa utaratibu maalum utakaotolewa na uongozi wa soko hilo.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila amezungumzia oparesheini ya kuwaondoa wafanyabiashara za ngono (Dada Poa) inayofanyika Wilayani Ubungo na kusema kuwa Mila,Desturi na Tamaduni za Tanzania hazikubaliani na biashara hiyo ya ngono pamoja na ndoa za jinsia moja hivyo Serikali mkoani humo itaendelea kupinga vitendo
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages