Breaking

Monday, 10 June 2024

DAWASA WABORESHA MIFUMO YA MAJITAKA MWENGE-ITV



Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) imeanza kazi ya kubadili bomba chakavu la Majitaka la inchi 16 na kuweka bomba jipya la ukubwa wa inchi 16 kwa umbali wa mita 90 likiendelea eneo la Mwenge ITV kwa lengo la kuboresha mifumo ya Majitaka iliyo na wateja zaidi ya 1,000.

Kazi hii inalenga kuboresha huduma ya usafi wa mazingira katika maeneo ya Mlimani city, Mwenge kwa masista, Mwenge round about, Mwenge TRA, Zahanati ya Mwenge pamoja na baadhi ya maeneo ya Sinza.





Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages