Breaking

Wednesday, 26 June 2024

MISA -TAN YAKUTANISHA WADAU SEKTA YA HABARI NA MAWASILIANO KUJADILI KANUNI ZA MAUDHUI YA MTANDAONI


Mkurugenzi wa MISA-TAN Elizaberth Riziki.

Na Marco Maduhu,Dar es Salaam


TAASISI ya Vyombo vya Habari Kusini Mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA-TAN) kwa kushirikiana na Protection International Africa (PIA) wamefanya Warsha na Wadau Sekta ya Habari na Mawasiliano, kujadili na kutoa maoni juu ya Kanuni za Maudhui ya Mtandaoni ya mwaka 2018.

Warsha hiyo imefanyika leo Juni 26,2024 Jijini Dar es salaam kwa Ufadhili wa Ubalozi wa Finland Tanzania.
Akizungumza kwenye Warsha hiyo Mkurugenzi wa MISA-TAN Elizaberth Riziki, amesema wamekuwa wakiendesha Warsha za namna hiyo ili kujadili Sheria mbalimbali za habari, ambapo mwaka jana walikuwa pia na Mjadala wa Sheria ya huduma za habari ya mwaka 2016, na mwaka huu wanajadili kuhusu Kanuni za Maudhui ya Mtandaoni ya mwaka 2018 na maboresho yake.

Amesema katika Mjadala huo wa Kanuni za Maudhui ya Mtandaoni 2018 utaibua mambo mengi, sababu wadau watajadili Kanuni hizo na kutoa maoni yao mbalimbali zikiwamo changamoto za sharia hiyo.
“Tunaishukuru Serikali kwa kuonyesha nia ya kubadilisha Kanuni za Habari, usiposhukuru kwa madogo huwezi kupewa makubwa,huu Mradi ambao tunafanya na Ubalozi wa Finland na Protection Africa tunataka kuongeza uelewa juu ya Kanuni ya Maudhui ya Mtandaoni ya mwaka 2018, kama tulivofanya mwaka jana kwenye Sheria ya huduma ya habari ya mwaka 2016,”amesema Riziki.

Mwezeshaji kwenye wa Warsha hiyo ambaye ni Mbobezi wa Masuala ya Sheria Deus Kibamba, amesema Kanuni ya Maudhui ya Mtandaoni ya mwaka 2018 ilitungwa ili kudhibiti uholela wa kusambaza Taarifa Mtandaoni.
“Tunapojadili Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta EPOCA (2010) inampa Waziri wa Sekta husika kutunga Kanuni itakayo ruhusu na kudhibu maudhui ya Mtandaoni, na Kanuni hizi zilitungwa mwaka 2018,”amesema Kibamba.

Amesema Wadau wa Habari na Waandishi wa Habari, wanapaswa kuijua kanuni hiyo ya Maudhui ya Mtandaoni pamoja na kuitekeleza wakati wa kusambaza taarifa ili wapate kuwa salama.
Ametolewa Mfano Kanuni ya 3 iliyorekebishwa kwamba hata kupokea Maudhui ambayo yapo kwenye utata na ukayasambaza ni kosa, na hata kutumia Mtandao wako kuchukua Maudhui hayo napo upo kwenye hatari, tatizo ambalo hufanywa na watu wengi katika kusambaza taarifa.

Aidha, amezungumzia pia kwa upande wa utoaji wa Lesseni za Muadhui ya Mtandaoni, kwamba kumekuwa na Masharti mengi ambayo yamekuwa yakisababisha upatikanaji wa Leseni kuwa mgumu.
“Kanuni hii ya Maudhui Mtandaoni ya mwaka 2018 ili kuja kudhibiti uholela wa kusambaza taarifa Mtandaoni,hata leseni zake zinaisha baada ya Miaka Mitatu, na kama Maudhui yako yalikuwa na shida siku ukienda kuhuisha leseni yako unabanwa na huenda usipewe, lakini Leseni za NGO zenyewe huisha muda wa miaka 10, hivyo leseni yako ikiwa ya muda mfupi ina maana hakuna uaminifu,”amesema Kibamba.

Naye Wakili Gideoni Mandes akizungumza kwenye Waesha hiyo , ameishauri Serikali kuona uwezekano wa kupunguza Ada za usajili vyombo vya habari vya Mtandaoni ili ziweze kuwa Rafiki, na hata vijana ambao wanatoka Vyuo wapate kuzimudu na kujiajiri.
 Patrick Kipangula kutoka Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali, amesema suala ya upunguzaji wa Ada za Usajili za Media za Mtandaoni tayari lipo kwenye mchakato wa kufanyiwa kazi.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkurugenzi wa MISA-TAN Elizaberth Riziki.
Mbobezi wa Masuala ya Sheria Deus Kibamba akizungumza kwenye Warsha hiyo.
Wakili Gideoni Mandes akizungumza kwenye Mkutano.
Afisa Program kutoka LHRC Raymond Kanegele akizungumza kwenye Warsha hiyo.
Patrick Kipangula kutoka Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali akizungumza kwenye Warsha hiyo.
Warsha ikiendelea.
Picha ya Pamoja ikipigwa.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages