Breaking

Wednesday, 12 June 2024

MAJARIBIO UFUNGAJI MITA ZA MALIPO YA KABLA YASHIKA KASI



Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) inaendelea kwa kasi na zoezi la ufungaji wa dira za majaribio za malipo ya kabla (pre-paid meters) ambapo hadi sasa dira zaidi ya 160 zimefungwa kwa wateja wakubwa na wadogo waliopo kwenye eneo la huduma.

Zoezi hili ni endelevu ambapo hadi sasa Mamlaka imefunga dira hizo katika hoteli kubwa, Taasisi za Serikali, Mabalozi na nyumba za viongozi wa Serikali katika Wilaya ya Kinondoni na Ilala.

Lengo kuu la kufunga dira hizo za majaribio ni kupima ufanisi wake kuelekea mabadiliko ya kuanza kutumia rasmi dira za huduma ya malipo ya kabla unaotazamiwa kuanza hivi karibuni.




Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages