Breaking

Sunday, 16 June 2024

DKT. BITEKO AVUTIWA NA HUDUMA ZINAZOTOLEWA TVLA

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko amevutiwa na huduma zinazotolewa na Wakala ya Maabala ya Veterinari Tanzania (TVLA) alipotembelea banda la TVLA siku ya kilele cha Maonesho na Mnada wa Mifugo 2024 yaliyofanyika kwenye shamba la Mkonge la Highland Estate Chalinze Ubena Zomozi Mkoa wa Pwani Juni 16, 2024.

Akiongea kwa niaba ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo Dkt. Benezeth Malinda alisema kuwa majukumu makubwa ya TVLA ni pamoja na kufanya utafiti wa magonjwa ya wanyama, kufanya uchunguzi wa magonjwa ya wanyama, kuzalisha na kusambaza chanjo za magonjwa ya Mifugo ambapo hadi sasa TVLA inazalisha aina 7 za chanjo.

Sambamba na hayo Dkt. Malinda aliongeza kuwa, mkakati wa Wizara kwa kushirikiana na TVLA imepanga hadi kufikia mwaka 2030 itakuwa inazalisha Chanjo 13 za kipaumbele na hadi kufikia sasa TVLA tayari imeshanunua magari ya mfumo wa baridi ambayo yanasambaza chanjo ambazo zimeshaanza kuzalishwa ili kuwafikia wafugaji kote nchini.

Mhe. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Serikali imetenga fedha kiasi cha shilingi bilioni 26 kwa ajili ya kuendesha kampeni ya chanjo kitaifa kwa lengo la kuhamasisha wafugaji kuchanja Mifugo yao ili kuzuia isishambuliwe na magonjwa kwani kuchanja Mifugo kutaongeza mazao ya Mifugo kukizi soko la nje ya nchi. Alisema Dkt. Malinda

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko aliongozana na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Alexandar Mnyeti (MB), Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora Mhe. Riziwani Kikwete, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe, Naibu katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Daniel Mushi pamoja na viongozi waandamizi wa Wizara
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko akipata maelezo kuhusiana na huduma zinazotolewa na Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo Dkt. Benezeth Malinda kwenye kileie cha Maonesho na Mnada wa Mifugo 2024 yaliyofanyika Juni 16, 2024 kwenye shamba la Mkonge la Highland Estate Chalinze Ubena Zomozi Mkoa wa Pwani.
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dkt. Stella Bitanyi akifuatilia hotuba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko (hayupo pichani) kwenye kilele cha Maonesho na Mnada wa Mifugo 2024 yaliyofanyika Juni 16, 2024 kwenye shamba la Mkonge la Highland Estate Chalinze Ubena Zomozi Mkoa wa Pwani.
Wataalamu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Afisa Utafiti Mifugo Bw. Msafiri Kalloka (wa kwanza kushoto) pamoja na Daktari Mtafiti wa Mifugo Dkt. Fredy Makoga wakitoa elimu kuhusiana na huduma zinazotolewa na TVLA kwa wadau wa Mifugo waliotembembela banda la TVLA kwenye kilele cha Maonesho na Mnada wa Mifugo 2024 yaliyofanyika Juni 16, 2024 kwenye shamba la Mkonge la Highland Estate Chalinze Ubena Zomozi Mkoa wa Pwani.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages