Breaking

Tuesday, 25 June 2024

DKT. ABBASI AWAONGOZA WATUMISHI KUMPOKEA NAIBU KATIBU MKUU MABULA



Na John Mapepele

Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi amewaongoza watumishi wa wizara hiyo kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Utalii, Nkoba Mabula aliyeteuliwa hivi karibuni baada ya kuwasili kwenye Ofisi yake mtumba Mtumba jijini Dodoma.

Mara baada ya kuwasili alipokewa na watumishi wote wa Wizara hiyo na baadaye kufanya kikao na menejimenti ya Wizara.

Akimkaribisha ili aweze kuzungumza na Menejimenti Dkt. Abbasi, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa maono yake ya kuboresha sekta ya utalii ambayo imekuwa na mchango kwenye uchumi.

Amemshukuru kwa kumteua Mabula ili aweze kusaidia sekta ya utalii ili kuimarisha na kuboresha sekta hiyo ambayo yeye mwenyewe amekuwa akiipambania.

"Kipekee napenda kumshukuru Mhe. Rais kwa kutuongezea nguvu katika eneo hili, sisi tunamshukuru na kumpongeza kwa maono yake makubwa kwenye sekta ya utalii kwani yeye mwenyewe amekuwa mwongoza Utalii namba moja. Akitoka ofisini akapanda milima na mabonde, akacheza filamu ya The Royal Tour " amefafanua Dkt. Abbasi

Katika hatua nyingine, Dkt. Abbasi amemkabidhi vitendea kazi ikiwa ni pamoja na miongozo mbalimbali kama sera na kanuni za sekta ya utalii.

Kwa upande wake, Mabula amewashukuru watumishi wote na kuomba ushirikiano ili kufanya kazi kwa weledi.



Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages