Zoezi hili linaenda sambamba na kutoa elimu ya matumizi sahihi ya maji, ulinzi wa miundombinu ya maji, pamoja na umuhimu wa kulipa bili za maji kwa wakati sambamba na kusitisha huduma kwa wateja wenye malimbikizo ya muda mrefu.
Mamlaka inaendela kuwasisitizia Wateja kulipa bili kwa wakati ili kuisaidia Mamlaka kuboresha zaidi huduma zake.




