Breaking

Tuesday 18 June 2024

BRELA YATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI WA MKOA WA DAR ES SALAAM

WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni(BRELA) imeamua kuwaandaa mafunzo maalumu kwa waandishi wa habari za biashara 44 kutoka vyombo mbalimbali vya habari kutoka Mkoa wa Dar es Salaam lengo likiwa kuwajengea uwezo utakaowezesha waandishi hao kuandika kwa weledi habari za Wakala huo.

Akizungumza leo Juni 18, 2024 jijini Morogoro wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo ya siku nne yaliyoanza Leo,Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni BRELA (BRELA) Godfrey Nyaisa amesema sababu za kuandaa mafunzo hayo ni utekelezaji wa maelekezo ya vikao vya Wakala huo.

Amefafanua kuwa wameanza na waandishi hao wa habari za biashara kutoka Mkoa wa Dar es Salaam na hasa wanaondika habari za BRELA lakini mikakati yao ni kwamba mafunzo hayo yatatolewa kwa waandishi wa Mikoa yote na lengo ni kuhakikisha wanaendelea kuwajengea uwezo wadau muhimu wakiwemo waandishi wa habari.

"Tumeamua kuandaa mafunzo haya baada ya kuona habari zinazohusu BRELA zina mambo mengi yakiwemo ya kisheria,hivyo ni vema waandishi wa habari tukawajengea uelewa na kuwawezesha kuwa na ufahamu wa kutosha wa kuandika habari zinazohusu taasisi hii .

"Tumeshuhudia baadhi ya habari ambazo zinaripotiwa lakini Zina makosa mengi,lakini tuona kinachohitajika ni elimu  ili kuondoa makosa hayo huku akisisitiza kwamba kupitia Wakurugenzi wa Wakala huo watatoa elimu ya kutosha katika mafunzo hayo na waandishi wa habari wasisite kuuliza kwa lengo la kujifunza zaidi,"amesema Nyaisa.

Aidha amesema mpango wa mkakati wa BRELA ni kuwa na kanzi data ya waandishi wa habari ambao watakuwa wanaandika habari za Wakala huo ili kusaidia kuwa na habari zenye usahihi na kwamba mafunzo hayo yanaendelea kutolewa sambamba na kuwaita katika matukio yanayohusu BRELA.

Pia amesema kuanzia sasa wataanza kutoa tuzo Maalum kwa waandishi wa habari za biashara ambao watakuwa wakiandika makala zenye matokeo chanya kwa jamii lakini makala ambazo zitakuwa zimejitosheleza.

"Tutakuwa na tuzo maalum kwa waandishi wa habari ambao watakuwa wanaandika Makala zinazohu BRELA.Tutakuwa tunashindanisha makala hizo na mshindi wa kwanza ambaye atakuwa ameandika makala Bora atapewa tuzo na itakuwa ENDELEVU,"amesema Nyaisa katika mafunzo hayo ambayo ni ya kwanza kutolewa na Wakala huo 

Kuhusu majukumu ya BRELA ni  pamoja na kusajili Makampuni, Majina ya Biashara, Alama za Biashara na Huduma, Viwanda vidogo, kutoa Hataza, Leseni za Biashara kundi A na Leseni za Viwanda. Menejimenti na Wafanyakazi wa BRELA, wapo tayari kukusikiliza na kutoa huduma bora ili kufanikisha lengo lako.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah akifungua Mafunzo ya Siku Nne ya BRELA kwa Waandishi wa habari ambao wanaripoti Mkoa wa Dar es Salaam, yaliyofanyika mkoani Morogoro.
,Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni BRELA (BRELA) Godfrey Nyaisa akizungumza wakati wa Mafunzo ya BRELA kwa Waandishi wa Habari wanaoripoti Mkoa wa Dar es Salaam, yaliyofanyika mkoani Morogoro.
Mwandishi wa habari wa Radio Uhuru, Elias Julius akizungumza jambo wakati wa Mafunzo ya Siku Nne ya BRELA kwa Waandishi wa habari ambao wanaripoti Mkoa wa Dar es Salaam, yaliyofanyika mkoani Morogoro.
Mwandishi wa habari wa TV E, Hellen Manyangu akizungumza jambo wakati wa Mafunzo ya Siku Nne ya BRELA kwa Waandishi wa habari ambao wanaripoti Mkoa wa Dar es Salaam, yaliyofanyika mkoani Morogoro.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah akiwa na viongozi wengine wakiwa kwenye picha ya pamoja na waandishi wa habari wa magazeti wakati wa Mafunzo ya Siku Nne ya BRELA kwa Waandishi wa habari ambao wanaripoti Mkoa wa Dar es Salaam, yaliyofanyika mkoani Morogoro.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah akiwa na viongozi wengine wakiwa kwenye picha ya pamoja na waandishi wa habari wa Redio wakati wa Mafunzo ya Siku Nne ya BRELA kwa Waandishi wa habari ambao wanaripoti Mkoa wa Dar es Salaam, yaliyofanyika mkoani Morogoro.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye Mafunzo ya Siku Nne ya BRELA kwa Waandishi wa habari ambao wanaripoti Mkoa wa Dar es Salaam, yaliyofanyika mkoani Morogoro.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages