WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni(BRELA) umetaja siri ya mafanikio yake ambayo yanaweza kufanya kazi zao bila kusabababisha usumbufu au taharuki kwa jamii.
Akizungumza leo Juni 18,2024 wakati akitoa mada kuhusu utoaji wa leseni za biashara kundi A, Mkurugenzi wa Leseni BRELA Andrew Mkapa ametumia nafasi hiyo kueleza namn ambavyo wanavyotoa huduma kwa mtazamo wa kirafiki zaidi na ndio maana ya wao kuwa Wakala kwa niaba ya Serikali.
Akifafanua zaidi Mkapa amesema “Kuna swali limeulizwa hapa kwanini hatuna kishindo na nini siri ya mafanikio yetu?BRELA tunatoa leseni za biashara ambazo kundi A zenye sura ya kitaifa na kimataifa, hivyo hatuna ofisi kule ngazi ya chini kabisa ingawa tunakwenda kutoa elimu kwa wananchi.
“Tunapokwenda mikoani tunashirikiana na maofisa biashara wanaohusika na kutoa leseni tunawapa elimu.Lakini siri ya mafanikio yetu ni kubadilika kimtazamo kwasababu nia mojawapo kubwa ya Serikali ilikuwa kubadilisha taasisi hizi ziwe wakala .
“Serikali ilitoa jukumu la kusimamia kwa niaba yao na lengo la kutoa nafasi kwa Wakala ilikuwa ni kupunguza urasimu.Hii imetusaidia katika kutoa huduma zetu.”
Hivyo Mkapa amesisitiza siri ya mafanikio yao na kutoa huduma kirafiki imetokana na kubadilika kwa fikra ndio kumeufanya Wakala huo kufanya kazi zake kiweledi.
Akifafanua kuhusu utoaji wa leseni za biashara kundi A amesema awali leseni hizo zilikuwa zikitolewa moja kwa moja na Wizara ya Viwanda na Baishara lakini baadae jukumu hilo lilihamishiwa BRELA.
Hata hivyo amesema katika idara ya utoaji leseni amesema kuna aina mbili za leseni ambazo zinatolewa na BRELA ikiwemo leseni ya biashara kundi A ambayo imekaa katika sura ya kitaifa na kimataifa.
Pia amesema huduma za BRELA kuanzia mwaka 2018/2019 zinatolewa kwa njia ya mtandao, hivyo mtu haijatajiki kwenda ofisi kwa ajili ya kuomba leseni ya biashara kwani huduma zinatolewa kwa njia ya mtandao.
Akieleza zaidi amesema wakati tujukumu la kutoa leseni kund A zinahahamishwa kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara tayari kulikuwa na mfumo uliobakia kidogo wa kukamilisha mfumo wa kutoa leseni za biashara kwa njia ya mtandao.
“Mfumo ulianza kutengenezwa wizarani na ulikuwa umefika hatua za mwishoni lakini na BRELA tulishaanza kutengeneza mfumo wetu kwa ajili ya kutoa huduma tulizokuwa nazo.
“Hivyo BRELA tulishakuwa na mfumo na ndio maana mfumo wa wizarani unatumika katika leseni za biashara za kundi A bado zinapatikana katika mfumo wa Tanzania National Bussiness Portal(TNBP) unaopatikana kupitia www.bussiness.go.tz .