Breaking

Wednesday 19 June 2024

ADA YA USAJILI WA LESENI YA KIWANDA INALIPWA MARA MOJA KWA UHAI WA KIWANDA- BRELA

NA EMMANUEL MBATILO, MOROGORO

WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imesema ada ya usajili wa leseni ya kiwanda ni Sh.800,000 na ada hiyo inalipwa mara moja kwa uhai wa maisha yote ya kiwanda lakini kwa upande wa Viwanda vidogo ada ya usajili ni Sh.10,000 na hiyo ni kwa muda wote.

Ameyasema hayo leo Mkurugenzi wa Leseni (BRELA), Andrew Mkapa akitoa wasilisho la Leseni za Viwanda pamoja na usajili katika Mafunzo ya Siku nne ya BRELA kwa Waandishi wa habari wanaoripoti Mkoa wa Dare es Salaam ambayo yanayoendelea mkoani Morogoro.

Amesema Viwanda vimegawanyika katika makundi mawili kwa mujibu wa Sheria ambapo kundi la kwanza ni viwanda vikubwa na vya kati ambavyo mtaji wake unaanzia Sh.milioni 100 na kundi la pili linahusisha viwanda vidogo ambavyo mtaji wake uko chini ya Sh.milioni tano.

"Leseni ya viwanda vikubwa ni Sh.800,000 , halafu kiwanda ambacho uwekezaji wake hauzidi hauzidi Sh.milioni ni sh 10,000, uwekezaji ambao unazidi ya Sh.milioni Tano ada yake ni Sh 50,000 na uwekezaji unaozidi Sh.milioni 10 ada yake ni Sh.100,000,"amesema.

Aidha amesema kuwa baada ya kiwanda kupewa leseni au kusajiliwa kila mwaka wahusika wanatakiwa kuwasilisha taarifa ya maendeleo ya kiwanda ambapo kuna fomu maalum ya kujaza ambayo inauliza maendeleo ya kiwanda.

"Na hii ripoti ya kiwanda ambayo inatakiwa kuwasilisha BRELA kila mwaka haina malipo katika kiwanda .Ni bure kama ukitoa taarifa ndani ya mwaka lakini ukichelewa ndio kuna faini ndogo kama Sh.10,000.

"Lakini tunaamanisha wenye Viwanda ambao wamepata leseni kutoa taarifa zao kwani zinasaidia kutunza kumbukumbu ambazo zinaweza kutumia na Serikali,"amesema na kufafanua ukisoma Ilani ya CCM lakini Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amekuwa akisisitiza taasisi za Serikali zisomane badala kuingia katika Mfumo mmoja.

"Hivyo na BRELA tumejiunganisha na mifumo ya taasisi nyingine lakini mfumo huo una matoleo mengine kwa taasisi inayotaka kuingia katika mfumo wetu ili kurahisisha huduma.Hata hivyo BRELA tumejipanga kuendelea kutoa huduma bora sambamba na kuendelea kurasimisha viwanda.

Pamoja na hayo ameeleza kuwa BRELA wameweka mkakati wao kwamba huduma yoyote ambayo watalifanya haitazidi siku tatu na kama ombi litakuwa limekamilika na hakuna maombi mengi kwa siku hiyo hata saa moja au mbili zinatosha kukamilisha huduma.
 Mkurugenzi wa Leseni (BRELA), Andrew Mkapa akitoa wasilisho lake la Leseni za Viwanda pamoja na usajili katika Mafunzo ya Siku nne ya BRELA kwa Waandishi wa habari wanaoripoti Mkoa wa Dare es Salaam ambayo yanayoendelea mkoani Morogoro.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye Mafunzo ya Siku nne ya BRELA kwa Waandishi wa habari wanaoripoti Mkoa wa Dar es Salaam ambayo yanaendelea katika Mkoa wa Morogoro.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages