Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kupitia watalaamu wa maabara imeendelea na zoezi la uchukuaji sampuli za maji na kufanya upimaji wa ubora Wilaya ya Ilala katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Lengo la zoezi hili ni kuendelea kuhakikisha ubora wa maji unaowafikia Wananchi ni safi na salama ili kuepuka na magonjwa ambukizi ikiwepo kuhara na magonjwa hatarishi.