Kukamilika kwa kazi hii kumeimarisha upatikanaji wa maji kwa wakazi wa maeneo ya Makabe polisi, Makabe serikali ya Mtaa, Kwa Washa, Efatha, Msamaria, Kwa Mzungu, Kwa Biligenda, Dubai, Nyota njema na Kwa Fungo wilaya ya Ubungo.
DAWASA inaendelea kuwasihi wananchi kutoa taarifa endapo watabaina uvujaji katika maeneo yao mawasiliano rasmi ya Mamlaka kupitia Kituo cha huduma kwa wateja kwa 0800110064(bure) na mitandao ya kijamii.




