Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe.Omari S.Shaaban amepongeza zoezi la ukusanyaji taarifa za Viwanda inayofanywa na Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO).
‘’Hili zoezi ni muhimu sana hakikisheni mnalikamilisha kwa wakati ili walengwa waweze kupata taarifa sahihi kwani maendeleo ya Viwanda nchini inategemea taarifa sahihi’’ aliongeza Mhe. Shaaban.
Mhe.Waziri alisema hayo alipofanywa ziara katika banda la TIRDO katika Viwanja wa Bunge ikiwa ufunguzi wa Maonesho ya wiki ya Viwanda inayofanyika kufuatia kwa Bajeti ya Wizara ya Viwanda na Biashara ilifanywa na Waziri Mhe. DR. Ashatu Kijaji katika Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utarafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) Prof. Madundo Mkumbukwa Mtambo alimhakikishia Mhe. Waziri kuwa zoezi litakamilika kwa wakati na kuelezea baadhi ya faida na mafanikio makubwa yatakayopatikana baada ya kukamilika kwa mpango wa kukusanya taarifa za Viwanda(Industria Mapping) pamoja na Mfumo wa utoaji taarifa za Viwanda NIIMS (National Industrial Information Management System )
Prof Mtambo amemueleza mgeni rasmi kuwa mfumo huo utakapokamilika utarahisisha upatikanaji wa taarifa sahihi za viwanda nchini pamoja na kutambua fursa zilizopo katika sekta ya Viwanda ambapo mpaka sasa zoezi hilo limeshafanyika katika mikoa mitano ambayo ni Dar es Salaam , Pwani, Morogoro, Tanga na Mkoa wa Kilimanjaro.
Prof. Mtambo amesema lengo ni kukamilisha zoezi hilo katika mikoa yote ili mwisho wa siku wawekezaji na wazalishaji wa malighafi za viwanda waweze kupata taarifa hizo kwa urahisi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TIRDO ambaye pia alikuwepo kwenye Maonesho hayo Mha.Bashiri Juma Mrindoko ameeleza kuwa taasisi yake imekuwa kinara wa utoaji wa tafiti za Viwanda na kuwataka wadau wa sekta ya Viwanda kufika katika Shirika hilo kupata taarifa za kitafiti zilizofanywa na wataalam. Mha.Mrindoko amezitaja baadhi ya tafiti zilizofanywa na wataala wa TIRDO kwa siku za hivi karibuni kuwa ni pamoja na uzalishaji wa mkaa mbadala kwa kutumia makaa ya Mawe pamoja na mabaki ya mimea, mtambo rahisi wa kuchakata mafuta ya Parachichi, Mtambo wa kukaushia mimea, samaki na nyama pamoja na uongezaji wa thamani wa zao la mihogo na zao la Mwani.
Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) ni a shirika la utafiti na maendeleo la taaluma mbalimbali lililoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Na. 5 ya 1979 na ilianza kufanya kazi tarehe 1 Aprili, 1979. Ni taasisi inayomilikiwa na Serikali chini ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
Jukumu lake ni kusaidia sekta ya viwanda Tanzania kwa kutoa utaalam wa kiufundi na huduma za usaidizi ili kuboresha zao msingi wa teknolojia. Zaidi ya hayo, mamlaka ya TIRDO ni kufanya utafiti uliotumika kwa ajili ya maendeleo ya teknolojia zinazofaa, na kuongeza thamani kwa rasilimali asilia kupitia usindikaji wa viwanda.