Breaking

Tuesday, 21 May 2024

TBS YASHIRIKI MAONESHO YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA DODOMA

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeshiriki katika maonesho ya wizara ya viwanda na Biashara katika viwanja vya Bunge yanayoendelea jijini Dodoma.

Wakiongea na maafisa wa TBS baadhi ya waheshimiwa wabunge waliotembelea banda la TBS wameipongeza TBS kwa kazi nzuri wanayofanya ya kuhakikisha usalama na ubora wa bidhaa unazingatiwa ili kumlinda mlaji wa mwisho.

Mkurugenzi Mkuu wa (TBS) , Dkt. Athuman Ngenya amewashukuru Waheshimiwa wabunge kwa kuweza kutenga muda wao kutembelea banda la TBS sambamba na kusikiliza wasilisho kuhusu majukumu ya Shirika na utekelezaji wake na kuahidi kutekeleza maelekezo yote waliyopewa kwa manufaa ya wananchi.

Maonesho hayo yamelenga kuwapatia fursa waheshimiwa wabunge kuongeza uelewa juu ya shughuli zinazofanywa na taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages