Breaking

Wednesday, 22 May 2024

PROF. SHEMDOE AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MWENYEKITI WA BODI YA PFCS

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe (kushoto) akipata ufafanuzi kutoka kwa MwenyekitI wa Bodi ya PFCS (Pig Farmers Co-operative Society) Bw. Dotto Eliuphoo kuhusiana na ushirika huo ulivyojipanga kujenga machinjo ya kisasa ya Nguruwe kwa lengo la kuongeza thamani ya nyama hiyo alipokutana nao kwenye ofisi ndogo ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi iliyopo Temeke Dar Es Salaam kwa lengo la kuomba kupatiwa eneo la ujenzi wa machinjio hiyo Mei 22, 2024.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe akitoa maelekezo kwa MwenyekitI wa Bodi ya PFCS (Pig Farmers Co-operative Society) Bw. Dotto Eliuphoo kuhusiana na aina ya machinjio inayohitajika ambayo itaendana na tekhnolojia iliyopo kwa sasa alipokutana nao kwenye ofisi ndogo ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi Temeke Dar Es Salaam kwa lengo la kuomba kupatiwa eneo la ujenzi wa machinjio hiyo Mei 22, 2024.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalilimbali kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na wajumbe wa Bodi ya PFCS (Pig Farmers Co-operative Society) waliomtembelea kwenye ofisi ndogo ya Wizara iliyopo Temeke Dar Es salaam kwa kwa lengo la kuomba kupatiwa eneo kwa ajili ya ujenzi wa machinjio hiyo Mei 22, 2024
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages