Breaking

Thursday, 16 May 2024

NEMC YATOA SIKU 90 KWA WENYE VITUO VYA AFYA KUWEKA MAZINGIRA WEZESHA YA KUTEKETEZA TAKA

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limetoa siku 90 kwa taasisi zote zinazojishughulisha na utoaji wa huduma za afya nchini kuweka miundombinu sahihi ya kuteketeza taka zinazotokana na huduma za afya au kuwapa wakandarasi waliothibitishwa na sheria ili kuepuka kuhatarisha afya na mazingira kwa ujumla.

Baada ya muda huo kupita NEMC watafanya ukaguzi kwenye vituo vya afya kuona utekelezaji wa agizo hilo na wale ambao watakiuka watachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kusimamishwa kutoa huduma mpaka watakapotekeleza agizo hilo.

Baraza hilo linakemea vikali tabia ya baadhi ya wafanyabiashara wa huduma za afya kuwapa taka watu ambao hawajaidhinishwa kutoa huduma hiyo na hatimaye kuzitupa hovyo jambo ambalo ni hatari kwa afya na mazingira.

Hayo yamebainishwa leo Mei 16, 2024 jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi wa Uzingatiaji na Ufuatiliaji Sheria NEMC, Hamad Taimuru wakati akitoa taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari kwenye Ofisi za NEMC.

Amesema usafirishaji na utupaji taka hizo hovyo bila kufuata miongozo na kanuni zilizopo unaweza kuleta athari kubwa kwa mazingira, binadamu pamoja na wanyama ikiwemo kuzuka kwa magonjwa mbalimbali na kupelekea hasara kubwa kwa Serikali ambayo itatumia fedha nyingi katika kudhibiti magonjwa na athari hizo.

"Ni dhahiri kuwa kuna baadhi ya watoa huduma za afya wasio waaminifu ambao wanakiuka matakwa ya Sheria ya Usimamizi wa Mazingira Sura ya 191 na Kanuni zake kwa kusafirisha na kutupa taka zinazotokana na huduma za afya bila kufuata utaratibu uliowekwa na Sheria pamoja na Wizara ya Afya ama bila kuwa na vibali vya Wizara husika". Amesema Taimuru.

Aidha amesema kuwa Baraza linazielekeza Mamlaka za udhibiti nchini zinazoshughulikia usimamizi wa taka zinazotokana na huduma za afya kuhakikisha kwamba watoa huduma za afya kote nchini wanafuata miongozo iliyowekwa na Wizara pamoja masharti ya Kanuni za Udhibiti na Usimamizi wa taka hatarishi za Mwaka, 2021 ikiwemo kuwa na miundombinu ya usimamizi wa taka zao pamoja na vibali vilivyotolewa na Wizara ya afya.

"Baraza litaendelea kusimamia kwa kushirikiana na vyombo na Mamlaka zote husika nchini kuweza kudhibiti ukikwaji huo wa Sheria. Kadhalika adhabu kali zitatolewa kwa wote ambao hawataweza kutekeleza agizo hili ikiwemo kufungiwa vituo vyao mpaka watakapoweka miundombinu madhubuti ya uhifadhi, usafirishaji na uteketezaji wa taka zao". Ameeleza.

Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004 kifungu cha 137 pamoja na kanuni za usimamizi wa taka hatarishi kanuni ya 52 mpaka 58 inaelekeza utaratibu wa usimamizi wa taka zinazotokana na huduma za afya ambazo ni vifaa vyenye ncha kali ikiwemo viwembe na sindano.
Kaimu Mkurugenzi wa Uzingatiaji na Ufuatiliaji Sheria NEMC, Hamad Taimuru akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 16, 2024 katika Ofisi za NEMC Jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa ya uwepo wa utupaji taka ovyo ambazo zinatoka katika hospitali na vituo mbalimbali vya afya

Kaimu Mkurugenzi wa Uzingatiaji na Ufuatiliaji Sheria NEMC, Hamad Taimuru akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 16, 2024 katika Ofisi za NEMC Jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa ya uwepo wa utupaji taka ovyo ambazo zinatoka katika hospitali na vituo mbalimbali vya afya.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages