Breaking

Tuesday, 28 May 2024

MRADI WA ASIA -AFRICA BLUETECH MKOMBOZI WA MAZAO YA UVUVI YANAYOPOTEA.

Na Mwandishi wetu

SEKTA ya Uvuvi nchini inakabiliwa na changamoto ya upotevu wa mazao ya uvuvi hivyo wadau wanatakiwa kuhakikisha wanatumia teknolojia za kisasa ambazo ni rahisi zitakazowezesha kukabiliana na changamoto hiyo.

Ameyasema hayo leo Mei 28, 2024, Jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Edwin Mhede wakati wa mkutano wa Uzinduzi wa mradi wa Asia -Africa BlueTech Superhighway ambao utachukua takribani miaka 7 (2024-2030) wenye lengo la kusaidia juhudi za serikali katika kupunguza upotevu wa mazao ya uvuvi.

Mkutano huo ambao umezikutanisha nchi nne Afrika, Dkt. Edwin Mhede amesema wamejielekeza kuhakikisha wanufaika wa mradi huo wanakuwa ni wavuvi wenyewe.

Pia amesema eneo ambalo wanalifanyia kazi kwa kushirikiana na Worldfish pamoja na Taasisi za ndani ni kuhakikisha wanakabiliana na changamoto za upotevu wa mazao ya uvuvi, pamoja na uharibifu mbalimbali unaojitokeza kwenye mnyororo wa thamani wakati watu wakivua, wakisafirisha, wakiuza na kununua samaki.

"Katika kutathimini fikra mpya za nini kifanyike zaidi ya hiki, tumejielekeza kuyagusa matatizo ya wavuvi na kujielekeza katika kufanya hivyo kuhakikisha kwamba mradi huu wanavufaika ni wavuvi wenyewe"

"Ni matumaini yangu baada ya siku kadhaa tutakuja kuwa na kitu kikubwa sana kuweza kutusaidia kuyafikia maisha ya wengi ambayo ndiyo maelekezo na ndiyo husara lakini pia ndiyo maono ya Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha tunaenda kuyakuta mahitaji ya watu na tunayafanyia kazi" amesema

Dkt. Mhede amesema changamoto nyingine zinazowakabili wavuvi hao, ni pamoja na uduni wa Teknolojia , upatikanaji masoko, upatikanaji wa mitaji ya kifedha na maarifa lakini pia miundombinu

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uvuvi, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Mohameed Sheikh, amesema Afrika ikiwemo Tanzania kunatatizo kubwa la upotevu wa mazao ya uvuvi ambapo inakisiwa kati ya asilimia 30-40 ya upotevu wa mazao hayo yanatokana na mabadiliko ya tabianchi

"Katika kipindi cha mvua inakua ni changamoto kubwa kwa wavuvi wetu hasa wale ambao wanachataka na wanasafirisha mfano, wavuvi wa dagaa wanavua na kuchakata, wanahitaji pia teknolojia mpya kwaajili ya kusarifu mazao yao ya uvuvi"amesema Prof. Sheikh.

Prof. Sheikh amesema serikali ya awamu ya sita imeendeela na jitihada za kuhakikisha wanaongeza uzalishaji wa mazao hivyo amewaomba wadau mbalimbali kuweka mbinu bora ambazo zitawasaidia wavuvi za kuweza kuhifadhi mazao yao ambayo yatakubalika ndani na nje ya nchi.

Naye Kiongozi wa Mawasiliano ya Kimataifa wa Taasisi ya WorldFish, Rajita Majumdar amesema kuwa zaidi ya tani 21.3 za samaki zimepotea kutokana na changamoto ya uhifadhi wa mazao hayo baada ya kuvuliwa ambapo wameona ni vyema kuja nchini kuisadia serikali na wavuvi kwa lengo la kupunguza upotevu huo ambao unahafifisha uchumi.

"Nadhani inahitajika matumizi ya teknolojia nafuu inayoweza kufikiwa ili kuongeza umahiri katika kushughulikia mnyororo wa usambazaji wa chakula ambapo itasaidia kuondokana na uharibifu mkubwa"amesema

Aditya Parmar ambaye ametoka kwenye Taasisi ya WorldFish,amesema mradi huo umejikita katika vipengele vinne ambavyo ni usambazaji wa samaki, uuzaji, utunzaji, uhifadhi na usafirishaji ambapo itasaidia kwa kiasi kikubwa kutunza thamani ya ubora chakula kwa lengo la kuhakikisha lishe bora kwa jamii ya pwani.

"Tunataka kuona jumuiya ya Pwani jinsi gani inaweza kuongeza mapato, tunataka kushirikisha wanawake na vijana kutekeleza mradi huu ambao tunatarajia utabadilisha maisha yao baada ya miaka michache ijayo "amesema

Mkutano huo unafuatiwa na mkutano ambao utafanyika Tarehe 5-7 mwezi Juni mwaka huu katika ukumbi wa Mikutano Mlimani city Jijini Dar es Salaam ambao unaozungumzia mahsusi wavuvi wadogo wanaochangia kwa asilimia 95.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Edwin Mhede akizungumza katika mkutano wa Uzinduzi wa Mradi wa Asia -Africa BlueTech Superhighway ambao utachukua takribani miaka 7 (2024-2030) wenye lengo la kusaidia juhudi za serikali katika kupunguza upotevu wa mazao ya uvuvi. Hafla hiyo imefanyika leo Mei 28, 2024, Jijini Dar es Salaam
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Edwin Mhede akizungumza katika mkutano wa Uzinduzi wa Mradi wa Asia -Africa BlueTech Superhighway ambao utachukua takribani miaka 7 (2024-2030) wenye lengo la kusaidia juhudi za serikali katika kupunguza upotevu wa mazao ya uvuvi. Hafla hiyo imefanyika leo Mei 28, 2024, Jijini Dar es Salaam
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Edwin Mhede akizungumza katika mkutano wa Uzinduzi wa Mradi wa Asia -Africa BlueTech Superhighway ambao utachukua takribani miaka 7 (2024-2030) wenye lengo la kusaidia juhudi za serikali katika kupunguza upotevu wa mazao ya uvuvi. Hafla hiyo imefanyika leo Mei 28, 2024, Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Uvuvi, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Mohameed Sheikh akizungumza katika mkutano wa Uzinduzi wa Mradi wa Asia -Africa BlueTech Superhighway ambao utachukua takribani miaka 7 (2024-2030) wenye lengo la kusaidia juhudi za serikali katika kupunguza upotevu wa mazao ya uvuvi. Hafla hiyo imefanyika leo Mei 28, 2024, Jijini Dar es Salaam
Mdau kutokaTaasisi ya WorldFish, Aditya Parmar akizungumza katika mkutano wa Uzinduzi wa Mradi wa Asia -Africa BlueTech Superhighway ambao utachukua takribani miaka 7 (2024-2030) wenye lengo la kusaidia juhudi za serikali katika kupunguza upotevu wa mazao ya uvuvi. Hafla hiyo imefanyika leo Mei 28, 2024, Jijini Dar es Salaam
Wadau mbalimbali wa uvuvi wakiwa katika mkutano wa Uzinduzi wa Mradi wa Asia -Africa BlueTech Superhighway ambao utachukua takribani miaka 7 (2024-2030) wenye lengo la kusaidia juhudi za serikali katika kupunguza upotevu wa mazao ya uvuvi. Hafla hiyo imefanyika leo Mei 28, 2024, Jijini Dar es Salaam
Wadau mbalimbali wa uvuvi wakizungumza jambo katika mkutano wa Uzinduzi wa Mradi wa Asia -Africa BlueTech Superhighway ambao utachukua takribani miaka 7 (2024-2030) wenye lengo la kusaidia juhudi za serikali katika kupunguza upotevu wa mazao ya uvuvi. Hafla hiyo imefanyika leo Mei 28, 2024, Jijini Dar es Salaam

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Edwin Mhede akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa uvuvi  wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa Asia -Africa BlueTech Superhighway ambao utachukua takribani miaka 7 (2024-2030) wenye lengo la kusaidia juhudi za serikali katika kupunguza upotevu wa mazao ya uvuvi. Hafla hiyo imefanyika leo Mei 28, 2024, Jijini Dar es Salaam

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages