Breaking

Monday, 20 May 2024

MKURUGENZI WA JENGA NA MIMI AFANIKISHA KUPATIKANA KWA SH. MIL 62.6 UJENZI WA NYUMBA YA MAPADRI KANISA KATOLIKI JIMBO LA KAHAMA

 

Mbunge wa jimbo la Ushetu , Emmanuel Cherehani akizungumza wakati Mkurugenzi wa Kampuni ya Uuzaji na Usambazaji wa Matofali na vifaa vya ujenzi maarufu Jenga na Mimi Investment Mhandisi Francis Mihayo akiendesha Harambee ya kukamilisha ujenzi wa nyumba ya mapadre Parokia ya Bikira Maria Mama wa Shauri Jema , Mbulu Jimbo Katoliki la Kahama Mkoani Shinyanga.
Mkurugenzi wa  Kampuni ya Uuzaji na Usambazaji wa Matofali na vifaa vya ujenzi maarufu Jenga na Mimi Investment Mhandisi Francis Mihayo akiendesha Harambee ya kukamilisha ujenzi wa nyumba ya mapadre Parokia ya Bikira Maria Mama wa Shauri Jema , Mbulu Jimbo Katoliki la Kahama Mkoani Shinyanga. Kushoto ni Mr & Mrs Alexander Kazimili wamiliki wa taasisi za Shule za Rocken Hill waliochangia bando 13 za bati
Mkurugenzi wa  Kampuni ya Uuzaji na Usambazaji wa Matofali na vifaa vya ujenzi maarufu Jenga na Mimi Investment Mhandisi Francis Mihayo 

Na Patrick Mabula , Kahama  

Mkurugenzi wa  Kampuni ya Uuzaji na Usambazaji wa Matofali na vifaa vya ujenzi maarufu Jenga na Mimi Investment Mhandisi Francis Mihayo amefanikisha kupatikana kwa kiasi cha shilingi Milioni 62.6 wakati akiendesha Harambee ya kukamilisha ujenzi wa nyumba ya mapadre Parokia ya Bikira Maria Mama wa Shauri Jema , Mbulu Jimbo Katoliki la Kahama Mkoani Shinyanga.

Fedha hizo zimepatikana Mei 19,2024  katika harambee aliyoendesha katika Parokia hiyo kwa lengo la kukamilisha ujenzi wa nyumba ya kukaa Mapadri kufuatia ile iliyopo kuchakaa kutokana na kuwa imejengwa tangu mwaka 1921 ilipoanzishwa kwa parokia hiyo.

Mhandisi Mihayo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika harambee hiyo amefanikisha kukusanya fedha hizo pamoja na vifaa vya ujenzi akiwa amesindikizwa na marafiki , ndugu , jamaa na waumini ambao kwa pamoja wamemuunga mkono na kufanikiwa kupata pesa hiyo pamoja na bando 13 za mabati aina ya Msouth na mifuko ya 100 ya saruji.

Akiongea na waumini , wageni mbalimbali waliokuwa wamealikwa katika harambee hiyo, Mhandisi Mihayo amewahamasisha kujitoa katika kulichangia kanisa ili watumishi wa Mungu , Mapadri waweze kupata nyumba nzuri ya kisasa ambapo patakuwa mahala pazuri kuishi katika utumishi wao.

Mhandisi Mihayo amesema mafanikio hayo yametokana na kuungwa mkono na marafiki , ndugu na jamaa na waumini wa parokia hiyo kutokana na kuwa nyumba wanayoishi mapadri wanaowatumikia wamekuwa wakiishi nyumba iliyopitwa na wakati kutokana na kujengwa toka mwaka 1921 ilipoanzishwa parokia hiyo na wamisionari wa Kizungu.

Awali kabla ya zoezi la harambee katika misa iliyoadhimishwa na Padri Jasten Msaiye wa parokia ya Familia Takatifu , Kagongwa, Jimbo la Kahama ambaye ni Dekano wa Dekania ya Mbulu kwenye mahubiri yake amewataka waumini kuendelea kuwa wamoja na kujitoa kulitegemeza kanisa na kuliunga mkono katika hatua ya maendeleo yake.

Katika Harambee hiyo Mhandisi Mihayo pekee amechangia zaidi ya Shilingi Milioni 10 huku Mbunge wa jimbo la Ushetu , Emmanuel Cherehani akimuunga mkono kwa kutoa mifuko 100 ya saruji na shilingi Milioni 2, Alexander Kazimil akitoa bando 13 za mabati geji 28 aina ya Msouth , huku marafiki , ndugu , jamaa na waumini wa parokia hiyo wakichangia milioni 52.6.

Paroko wa parokia hiyo Peter Kadundu katika hotuba yake amewashukuru wote waliojitoa kufanikisha harambee hiyo hususani Mhandisi Mihayo kwa moyo wake mwema kwa kukubali kuwa mgeni rasmi na kufanikisha kukusanya kiasi cha sh milioni 62.6 na kufanya wavuke lengo la shilingi Milioni 50 zilizokuwa zinahitajika kukamilisha nyumba hiyo ambayo boma lake lilishakamilika.
Meneja wa TCRA Kanda ya Kaskazini Mhadisi Francis Mihayo akizungumza wakati akiendesha Harambee ya kukamilisha ujenzi wa nyumba ya mapadre Parokia ya Bikira Maria Mama wa Shauri Jema , Mbulu Jimbo Katoliki la Kahama Mkoani Shinyanga.






























Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages